Jinsi ya kupika pilau kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika pilau kwa ajili ya biashara

 

Na Aisha Lungato

Moja ya biashara ambayo inalipa sana siku hizi na inafanywa na vijana wengi wa kiume nyakati za usiku ni uuzaji wa chakula haswa pilau.

Waswahili wanasema ‘kazi ni kazi ilimradi mdomo uende kinywani’ hivyo basi ukiamua kufanya jambo kwa ajili ya kukuingizia kipato lifanye kwa juhudi na bidii usiangalie watu watazungumza nini.

Pia kabla haujaanza biashara unatakiwa kutafuta sehemu yenye mzunguko wa watu wengi nyakati za usiku mfano Kariakoo, Buguruni, Kigamboni Feri na sehemu nyinginezo, unachotakiwa kukifanya ni kupika chakula kwa usafi kuhusu wateja watakuja tu.

Siku zote kwenye biashara kuna ugumu na urahisi wake utakapopata sehemu ambayo utafanyia biashara usikurupuke kupika vyakula vipi anza hata na kilo mbili kwa siku uangalie upepo ulivyo.

 

Mahitaji

 • Mchele kilo 2 ¼
 • Nyama kilo 1 ½
 • Mafuta ya kupikia robo
 • Njegere kilo 1
 • Giligilani fungu moja
 • Mdalasini nzima packti ndogo 2
 • Chumvi itakayotosha kwenye mapishi yako
 • Vitunguu maji 4 vikubwa
 • Vitunguu saumu 3
 • Hiriki nzima pakti 3
 • Unga wa pilau kiasi usiweke mwingi sana kwa sababu asilimia kubwa ya watu hawapendi pilau liwe jeusi.
 • Viazi vya chipsi hata ukipata 10
 • Karoti na hoho 2

 

Hatua inayofuata ni matayarisho ya viungo vyako anza kwa kuchemsha nyama yako ikiwiva weka pembeni na uanze kumenya na kukatakata vitu vyako kama vile vitunguu, kutwanga vitunguu swaumu, kuchambua mchele nk.

 

 

 

 

Anza mapishi yako sasa

 • Bandika sufuria yako jikoni iwe kubwa epuka kupika sufuria ndogo huwenda mchele unaotumia ukawa unavimba .
 • Weka mafuta ya kula ya kutosha, kwani siku zote pilau huwa linatumia mafuta mengi.
 • Kisha weka vitunguu vya kawaida na uviache mpaka viwe na rangi ya brown kisha tia nyama na uiache ijikaange vizuri.
 • Nyama yako ikiwa sawa weka kitunguu swaumu, hiliki, mdarasini, pamoja na unga wa pilau koroga taratibu
 • Kisha chukua viazi pamoja na mchele wako weka koroga tia mchuzi wa nyama uliobaki, au maji ya moto usisahau kuweka na chumvu.
 • Subiri vikauke kidogo vikishakauka chukua karoti na hoho ziweke kwa juu na uache uchemke mpaka ukaukie kabisa
 • Ukishakauka angalia kama maji uliyoweka yanatosha ua chakula chako bado kigumu ongeza maji kidogo chukua foili weka kwa juu hii ni kwa ajili chakula chako kiive na mvuke zaidi, funika weka moto mdogo juu na chini.
 • Mpaka kufikia hapo kazi yako itakuwa ni kuangalia chakula chako kama kimeiva kikiiva kiache jikoni kwenye moto mdogo kwa ajili ya wateja wako wakija wakute chakula cha moto muda wote.

Kama tujuavyo pilau bila kachumbari halinogi kabisa, ili kunogesha mlo wa wateja wako unatakiwa kukata kachumbari ya viwango ambayo haina mambo mengi kabisa, mpaka kufikia hapo kazi yako itakuwa ni kusubiri wateja tuu, lakini usafi muhimu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post