Jinsi ya kupika mchemsho wa ndizi

Jinsi ya kupika mchemsho wa ndizi

Na Aisha Lungato

Ndizi ni moja ya chakula kinachopendwa sana na watu wengi, lakini kwa hapa nchini chakula hiki huongoza kwa kuliwa zaidi na watu wa kabila la Wahaya kutoka mkoa wa Kagera, Bukoba. Sasa leo kwenye Nipe dili bwana tutapeana madini jinsi ya kupika  ndizi mchemsho twende sawa.

MAHITAJI

Nyama robo

Ndizi mzuzu mbichi 5 au kulingana na ukubwa wa familia yako

Vitunguu maji

Giligiliani vijani kiasi

Vitunguu swaumu

Rosemary (vijani vichache)

Bay (vijani kiasi)

Karoti

Chumvi

Oliver oil kijiko cha mezani kimoja

Black pepper

Chills endapo unapenda

Namna ya kuandaa

Menya ndizi zako na uzioshe vizuri kwa maji safi na salama.

Katakata vitunguu maji, na karoti kwa mtindo uupendao

 

Jinsi ya kupika

Chemsha nyama na ikiashaiva vizuri weka chumvi kiasi, bay, rosemary, black paper vyote hivi utaweka wakati nyama ikiendelea kuchemka.

Nyama ikishaiva vizuri weka vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na nndizi kisha acha viive vyote kwa pamoja, lakini kabla ya kutoa weka karoti.

Baada ya dakika 5 unaweza kutoa chakula motoni na kitakuwa ni tayari kimeiva na unaweza kula mchana au usiku pia.

Aiseee hii ndiyo nipe dili bwana yaani lazima mate yadondoke sio poa enjoy kile ulichokiandaa bhana!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post