Moja ya chakula rahisi kukiandaa ni Makaroni huku kikiwavutia wengi hasa watu wanaokaa wenyewe (Bachela). Licha ya chakula hicho kupendwa na wengi lakini baadhi yao hukosea kukipika.
Makaroni na pasta kwa jumla ziliandaliwa na kutumika hasa na watu wa Italia, lakini kwa muda zimekuwa chakula cha kawaida duniani kote. Awali chakula hicho kilipendelewa kuliwa katika sikukuu za Krismasi na Pasaka kutokana na uandaaji wake kuwa rahisi.
Kutokana na chakula hicho kuwa na uhitaji mwingi duniani na kwenye baadhi ya migahawa. Leo tumeangazia namna ya kuandaa chakula hicho ambacho unaweza kutengeneza kwa ajili ya kula mwenyewe nyumbani au kuuza kama biashara.
MAHITAJI
- Pakti ya makaroni 1 au 2
- Nyama ya kusaga nusu
- Kitunguu swaumu kilichosangwa vijiko viwili
- Pilipili mtama iliyosagwa kijiko kimoja
- Chumvi kiasi
- Nyanya 3 za kawaida
- Nyanya paste 1
- Brokoli 1 (ukipenda sio lazima kuweka)
- Karoti, hoho, na kitunguu cha kawaida
- Soya source vijiko viwili
- Kotmiri
- Pia unaweza kuweka viazi mbatata
- Limau au ndimu
Baada ya kuandaa vitu vyako vyote basi utatakiwa kuvikatakata ili unapoanza kupika kazi yake iwe ni kuweka jikoni pamoja na kukoroga tuu.
JINSI YA KUPIA CHAKULA CHAKO
- Anza kwa kuchukua sufuria yako kisha weka jikoni, weka maji kiasi, chumvi na pilipili mtama.
- Baada ya hapo subiri maji mpaka yachemke kisha tia Makaroni yakoroge na uache yachemke mpaka yaive (kwenye packi wameandika uchemshe kwa dakika 15 hadi 20 lakini kwa muda huo yanaweza yasewe tayari hivyo wewe utasubiri mpaka yaive kabisa).
- Ukishaona yameiva yaepue chukua chujio, chuja na uyaoshe na maji mengine halafu yaweke pembeni.
- Baada ya kumaliza utachukua sufuria yako nyingine utaweka mafuta kiasi kisha kitunguu utakaanga mpaka kiwe brown, halafu utaweka vitunguu swaumu utaacha vichemke kisai.
- Ukiona vitunguu vyako vipo sawa chukuwa nyama yako ya kusaga tia ongezea na limao au ndimu acha vichemke kwa muda kisha weka nyanya za kawaida halafu nyanya ya paste. Kisha utaacha mpaka nyanya zako ziive kabisa.
- Nyanya zikiiva weka brokoli, viazi, chumvi karoti, hoho na uache vichemke kiasi kisha chukua makaroni yako yaweke kwenye rosti ya nyama na uanze kukoroga.
- Utaongezea kotmiri na soya source, utaonja kama kila kitu kipo sawa basi utaipuna. Chakula chako kitakuwa tayari kwa ajili ya kula pamoja na kuuza.
Leave a Reply