Jinsi ya kupika futari ya mzinga wa nyuki kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika futari ya mzinga wa nyuki kwa ajili ya biashara

Na Aisha Lungato

 

Ni matumaini yangu wazima wa afya, kama tulivyozungumza wiki iliyopita mwendo ni ule ule tunapeana ma-deal na tips za futari,  leo tumekuja na futari ya ‘Mzinga wa Nyuki’.

Vipi unaujua mzinga wa nyuki au nimekuchanganya kidogo?, basi mzinga wa nyuki ni kitafunwa ambacho kinapikwa na kutengenezwa kama mkate wa skonzi lakini huu unakuwa tofauti kidogo kutokana na kuwekewa shira juu yake.

Mzinga wa nyuki ni mkate ambao katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani umekuwa ukipendwa na watu wengi kutokana na kuwa kitafunwa chepesi ambacho hakina mambo mengi, sasa wewe mfanyabiashara unaweza kujichukulia fursa hii na ukaigeuza kuwa biashara yako kwani kwa kipindi hichi kuna wateja wengi.

Nimekushushia fursa hii ambayo kwa bei inaanzia elfu tano na kuendelea, sasa ungana nami mwanzo mpaka mwisho kujia jinsi ya kutengeneza…

Mahitaji

      Unga - vikombe 3 ½ ambavyo havijajaa sana

      Maziwa fresh kikombe kimoja

      Maji  kikombe ½

      Yai - 1

      Sukari  vijiko 2 ½ vikubwa

      Mafuta nusu kikombe

      Hiriki ya unga nusu kijiko

      Hamira nusu kijiko cha chai

      Chumvi  robo kijiko cha chai

Jinsi ya kutayarisha na kupika

      Chukua bakuli kubwa weka vitu vyako vyote na uanze kukanda unga taratibu mpaka uwe mlaini kabisa mfano wa ngano ya chapati na uache kwa muda

      Kisha pakaza siagi juu na chini katika chombo chako cha kupikia

      Anza kukata unga wako viduara vidogo vidogo (angalizo visiwe vidogo sana) na uvipange katika chombo chako cha kupikia bila kuacha nafasi.

      Ukishamaliza process hiyo acha mkate wako uumuke kwa dakika 15 mpaka 30

      Kisha pika katika oven kwa moto wa kawaida na uache uive kwa dakika 25-30

Mkate wako ukishaiva utoe katika oven na uanze kutengeneza shira kwa ajili ya kumwagia juu ya mzinga wa nyuki. Sasa hapo kuna shira ya maziwa pamoja na ya kawaida kama ile ya kuweka kwenye visheti

Mahitaji ya Shira

      Sukari vikombe 2

      Maji kiasi

      Zaafarani nusu kijiko cha chai (iloweke)

      Maziwa fresh kikombe kimoja

Weka sufuria jikoni tia sukari, maziwa pamoja na maji kiasi, acha vichemke mpaka vitengeneze rojo kabisa, mpaka kufikia hapo shira yako itakuwa tayari kwa kuimwagia katika mkate wako.

Cha kunzingatia: katika umwagaji wa shira unatakiwa kufuata process hizi, kama shira yako ya moto basi utamwagia kwenye mkate uliopoa na kama shira yako imepoa utamwagia kwenye mkate wa moto. Yaani inatakiwa kimoja wapo kiwe kimepoa epuka kuweka vyote vikiwa vya moto.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags