Jinsi ya kupika donati za sukari ya kuganda

Jinsi ya kupika donati za sukari ya kuganda

Uhali gani! mchakarikaji mwenzangu, mwisho wa mwezi huu embu tukae kidogo tuulizane umeingiza shilingi ngapi mwezi huu? au ndiyo patupu na upo tuu hapo hutaki kujishughulisha.

Kama kawaidia yangu binti wa watu mie sichoki kuwaelewesha kuhusiana na maswala ya biashara, sasa leo nimekuja na biashara ya kitafunwa ambacho siku za hivi usoni watu wamekuwa wakikinakshi na mapambo mbalimbali kama vile ice sugar na chocolate, kitafunwa chenyewe ni donate.

Donate ni kitafunwa ambacho unaweza kunywea chai au kunya na soda au juice ni vile tuu wewe upendavyo, na biashara hii bwana unaweza kuifanya katika stande za bus, shuleni na hata kwenye maofisi. Sasa nisiongee sana ungana nami mwanzo mpaka mwisho kujua dondoo hii.

 

 

MAHITAJI/VIPIMO

  • Unga mweupe wa ngano (PPF) vikombe vikubwa 2 1⁄2
  • Siagi vijiko 2 vya chakula
  • Hamira vijiko 2 hapa kwenye hamira utatumia vijiko vile vidogo vya sukari vile bila kusahau baking poda kijiko kimoja
  • Mayai 2
  • Nazi ya unga
  • Maji kikombe11⁄3
  • Mafuta ya kukaangia

 

JINSI YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1- Ikiwa hamira ni ya kuumua haraka (instant yeast) weka vitu vyote pamoja katika bakuli uchanganye vizuri uwe mlaini kama wa mkate na sio mlaini sana kama wa kalimati.

2-Ukimaliza kukanda funika mchanganyiko wako uache uumuke kwa muda kisha anza kutengeneza duara zako za donat.

3- Weka mafuta yako jikoni yaache yapate moto kiasi, anza kukaanga donati zako, kisha epua zichuje mafuta kisha mwagia sukari au shira uliyotayarisha.

 

Jinsi ya kutengeneza hiyo shira yenyewe sasa

  • Sukari vikombe 2 utatumia vikombe vidogo
  • Maji 1⁄2 kikombe
  • Hiliki kijiko 1 cha chai

Kutengeneza shira: weki maji, sukari na hiliki kwa pamoja kisha weka jikoni ichemke huku ukiwa unakoroga bila kupumzika mpaka itakapo kuwa nzito ukiigusa inanata kama asali

Epua ipowe kisha imimine katika donuts uchanganye changanye mpaka shira igeuke sukari nyeupe ya kuganda (glazed) na hapo donate zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags