Jinsi ya kupika cupcakes kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika cupcakes kwa ajili ya biashara

Hey hey mko byee, mwendo ni ule ule tuchakarike jamani, tufanye kazi si mnajua tena bila kuchakarika maisha hayawezi kwenda kama tunavyotaka, sasa hii biashara ninayowalete leo ni bonge la biashara na lina faida sana.

Kama tunavyojua cupcake ni cake ambazo zinapendwa na kila rika na mara nyingi watu hutumia wakati wakiwa safarini kama chakula chao mpaka watakapo fika waendako.



Wacha niwaibie siri moja, hii biashara ukiianzisha kwa utulivu kabisa na akili zako timamu utapiga pesa nyingi sana, kwa mfano ukaamua kwenda kuungana na mabasi yako matano yanayokwenda mikoani uwe unauza cake zako au kwa yale mabasi yanayotoa chakula bure unaweza kuingia nao mkataba na ukajua watakulipa bei gani ambayo haitakuwa na hasara kwako na kwao.

Sasa tuje katika pishi letu la leo ni cupcake jamani msipuuzie huu unyama mtakuja kunishukuru baadaye.

MAHITAJI
 Siagi vikombe vitatu na robo
 Sukari kikombe kimoja na nusu
 Mayai 2
 Vanilla vijiko 2 vya chai
 Baking powder vijiko viwili na nusu
 Chumvi 1⁄4 KiJiko vya chai
 Unga wa ngano vikombe viwili na nusu
 Maziwa ya maji kikombe kimoja na nusu

JINSI YA KUTENGENEZA/KUOKA
 Chukua bakuli lako siyo kubwa sana la kiasi tu chekecha unga, chumvi pamoja na baking powder, koroga changanya vizuri kisha weka pembeni.

 Katika bakuli jingine weka siagi na ikoroge hadi iwe laini, tia vanilla na sukari kisha changanya tena hadi mchanganyiko uwe mweupe.


 Tia yai moja baada ya jingine huku unachanganya vizuri kila unapotia yai.

 Kwa kutumia mwiko au spatula tia unga kidogo kidogo pamoja na maziwa.


 Washa ovener joto 175°c. Tia paper liners katika muffin tins au paka mafuta kila tundu la muffin tray. Hapa sasa unawasha ovener au jiko la mkaa mapema ili kuacha jiko lipate moto vizuri ndiyo uendelee na mambo mengine.

 Mimina mchanganyiko wako katika muffin tins kisha oka hadi ziwe rangi ya brown.
 Zitoe jikoni kisha acha zipoe kabisa, hapa sasa unaweza kupambia kwa icing sugal uipendayo.

Pishi hili jamani sio gumu kiivyo, cha muhimu cha kuzingatia kwa wenzangu wa majiko ya mkaa inabidi tuu ujipinde ununue ovener maana cake hizi sina imani nazo kupikia kwenye jiko la mkaa, kwanza jiko la mkaa litakuchelewesha kwa sababu utaweka cupcake ngapi mpaka umalize kuoka so tumia ovener kuokoa muda na kupika kitu chenye ubora wa hali ya juu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags