Jinsi ya kupika Bagia za Kunde

Jinsi ya kupika Bagia za Kunde

Mambo vipi? mfuatiliaji wa Mwananchi scoop, karibu kwenye ukurasa wa nipe dili na leo tutakwenda kuelekezana jinsi ya kuandaa bagia za kunde je umeshawahi kujaribu kutengeneza?

Basi bila shaka fuatilia kwa makini mkubwa sana ili uweze kujifunza zaidi, bagia za kunde hua zinapendwa sana na watu hivyo ni fursa hii kwako kuweza kukuongezea kipato mtu wangu twende sawa.

Mahitaji muhuimu wakati wa kuandaa bagia za kunde.

  • Vikombe 2 kunde
  • Kitunguu 1 kikubwa
  • Pilipili kichaa 2 (nyekundu na kijani ukipenda)
  • Vijiko 3 vya chakula maji ya limao (ukipenda)
  • Kijiko 1 cha chai baking powder
  • Vijiko 1½ vya chai tangawizi
  • Kikombe ¼ majani ya giligilani
  • Chumvi kwa kuonja
  • Mafuta ya kukaangia

 

Jinsi ya kupika

  • Hakikisha unaosha na kuloweka kunde kwenye maji ya moto siyo chini ya masaa 8, au usiku mzima.
  • Baada ya hapo sasa katakata kitunguu, pilipili, majani ya giligilani; twanga tangawizi halafu weka pembeni.
  • Ukimaliza hapo chuja kunde zako maji
  • Weka kunde, maji ya limao na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula au blender ila isilainike sana.
  • Halkadhalika unaweza kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu.

 Zikilainika, ongeza kitunguu na majani ya giligilani kwenye mchanganyiko, saga kwa sekunde kama 20.

  • Hakikisha vitunguu na majani ya giligilani hayasagiki kabisa.
  • Ukimaliza hapo weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa.
  • Ongeza chumvi na baking powder, changanya vizuri
  • Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani.
  • Yakichemka, tumia vijiko 2 au mikono kutengeneza umbo kama la yai au umbo la bagia
  • Weka kwenye mafuta, Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia

Toa bagia zilizoiva kwenye mafuta.

  • Hamishia kwenye sahani/bakuli iliyowekewa tissues, au tumia chujio la bati ili mafuta yajichuje.

 Hapo sasa bagia zako zitakua tayari kwa kuliwa, kikubwa zingatia maelekezo ili uweze kutoa kitu kizuri kila la kheri mtu wangu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags