Jinsi ya kuongeza thamani yako ukiwa chuoni

Jinsi ya kuongeza thamani yako ukiwa chuoni

Na Michael Onesha

Mtu wa kwanza kutambua na kuamini kuwa wewe ni wa thamani kubwa ni wewe mwenyewe. Rule namba moja ukiwa kama kijana wakike au wa kiume unatakiwa kujiona wa thamani kubwa usikubali watu wakuaminishe kuwa wewe ni mtu wa kawaida usiye na thamani yoyote.

Maisha ya binadamu mwenye ufahamu timamu, mwenye kufahamu kwa nini anaishi na mwenye nia ya kufanikiwa lazima yawe na mwelekeo wa ukuaji pamoja na kutambua thamani yake.

Na leo katika segment yako kambambe kabisa tumekusogeza mada ambayo nafikiri kila mwanafunzi atakaye isoma basi itaweza kumuinspire kwa namna moja ama nyingine nayo ni namna au jinsi ya kuongeza thamani yako uwapo chuoni.

Fanya haya kuongeza thamani yako

 

  1. Badili mwenendo wako.

Maisha ni mchezo wa makosa, hakuna anayeweza kuifikia hatua fulani ya maisha bila kukosea, na kufanya makosa ni sehemu ya maisha. Jambo muhimu ni kuepuka kurudia makosa yenye kugharimu.

Ikiwa una mazoea uliyojijengea au tabia ambayo imekuletea hasara mara kadhaa fikiria kuachana nayo, mfano mzuri kwa wanafunzi wa vyuo mambo ambayo yanawarudisha nyuma kimaisha ni mikumbo ili uwe na thamani inabidi kubadilika mwenendo wako.

 

  1. Kugundua na kuendeleza kipaji chako.

Moja ya jambo kubwa ambali litakupa thamani kuliko unavyotegemea ni kugundua kipaji chako na kukitumia ili kutimiza ndoto yako.

Kipaji ni uwezo wa kufanya kitu fulani vizuri zaidi ya wengine, kila mtu Mungu amempa kipaji chake, kila mtu ana uwezo ambao mwingine hana kugundua kipaji chako ni nusu ya kugundua sababu ya Mungu kukuumba.

Wapo baadhi ya wanafunzi wenzako ambao wako chuo lakini ni mafundi wazuri wengine wafanyabiashara wazuri hivyo basi acha kuona wenzio hawana maana jaribu na chako uone thamani utakayopewa katika jamii inayo kuzunguka.

  1. Mafanikio yako yaguse maisha ya wengine

Mwanamuziki wa kimarekani Ricky Ross, amewahi kusema "kipimo cha mafanikio yako si tu kuangalia vitu vingapi unamiliki bali ni kuangalia watu wangapi wamenufaika na mafanikio yako". Jifunze kufikiria kuhusu wengine kwa vichache ulivyobarikiwa navyo.

Kuna watu wanahitaji masaada wako, hilo lazima ulikumbuke. Huwezi saidia wote lakini inatosha ukitumia ulichonacho kuwasaidia hata watu wachache kadiri ya uwezo wako.

Wengine hawahitaji fedha, wanahitaji neno la faraja na maarifa tu kutoka kwako usiwakimbie. So baadhi ya thamani za watu huonekana kutokana na matendo yao mema ukiwa kama mwanafunzini vyema kufanya jambo kwa uwezo wako.

  1. Jifunze vitu vipya.

Kila siku jifunze vitu vipya usiitumie siku yako kwa kupiga soga na kuchati kwenye mitandao katika mambo yasiyo na faida. Maisha yanataka ujioe muda wa kutafakari na kujifunza vitu vipya kila siku. Hii itakusaidia kujuana na watu sahihi watakao kuonesha njia za kupita ili uweze kufanikiwa.

  1. Ongeza bidii

Chochote kile unachokifanya kifanye kwa kumaanisha na kwa bidii mambo yanaweza kushindikana lakini wewe zidisha bidii mpaka yatokee.

Watu wenye kufanya mambo kwa kumaanisha na kwa bidii huheshimika sana hakuna jamii ambayo ni kipenzi cha watu legelege na wavivu, maisha ni kumaanisha na kujibidiisha.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post