Jinsi ya kukiri makosa yako kazini

Jinsi ya kukiri makosa yako kazini

Ooooh!!! yes, ni week nyingine tena ambapo tunakutana kupitia kipingele cha makala za kazi, ajira, ujuzi na maarifa kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu sector hii ya ajira.

Kama unavyofahamu sector hii bwana imegubikwa na mambo kadha wa kadha lakini je uliwahi kukosea mahali pako pa kazi halafu ukawa huelewi je ukiri kosa au ukomae tu na kiburi chako kama hakujatokea kitu?

Nataka kukujuza tu kitu kuwa neno samahani ni dogo sana ila limemeba uzito mkubwa kama utalisema kwa kumaanisha, hivyo unapokosea mtu sehemu yoyote ile huna jinsi kumuomba msamaha mtu huyo.

Acha leo nikuelekeze jambo ninauhakika litakutoa hofu na wasiwasi kabisa endapo itatokea umefanya kosa katika sehemu yako ya kazi.

Nikwambie tu kuwa makosa hutokea na hakuna haja ya kuzungumza uongo na kukosea kila mtu anakosea hakuna bianadamu mkamilifu.

Unapoweza kukiri makosa yako, badala ya kujaribu kuficha au kumlaumu mtu mwingine kwa makosa yako, una nafasi nzuri zaidi ya kujifunza kutokana na kosa hilo.

Ni kweli, utamaduni wa mahali pako pa kazi unaweza kuamuru jinsi makosa yanavyoshughulikiwa, lakini binafsi hupaswi kuishi kwa hofu ya kufanya makosa kwa sababu mvutano huo utajenga tu mazingira ambayo kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa.

Unachotakiwa kukifanya ukikosea mahala pa kazi…

KWANZA: Kubali kuwajibika kwa kosa kama kosa linaletwa kwa mawazo yako. Utapata imani na utetezi kutoka kwa wenzako na ‘timu’ ya wasimamizi, pia utaweka sauti ya mawasiliano ya wazi ya siku zijazo katika eneo lako la kazi.

PILI: Tathimini ni wapi ulikosea unapogundua kosa lako mwenyewe na kisha lifikishe kwa meneja wako badala ya kutumaini kuwa hakuna mtu anayegundua waswahili wanasema nenda kajifunge mwenyewe, lakini hii itakusaidia sana kuliko kukaa kimya mambo yakaendelea kuwa mabaya.

Unapo ripoti hitilafu, unaweza kueleza mahali ulipofanya kosa na kuleta mapendekezo ya jinsi unavyoweza kuepuka tatizo katika siku zijazo au kuomba ushauri kwa wafanyakazi wenzio na hata kwa meneja.

 TATU: Sikiliza kwa makini ukosoaji unaoweza kutarajia unapokubali kosa lako, bila kuhisi hasira au kutupia mtu lawama. Badala yake, endelea kuwa wazi kwa kujifunza somo kutokana na uzoefu. Ukosoaji unaojenga ni muhimu kwa ajili ya kujifunza.

NNE: Omba msamaha kwa kosa lako kwa kila mtu aliyeathiriwa na uweke ahadi ya kulirekebisha kwa uwezo wako wote. Bila kutoa visingizio, shiriki mawazo na mipango yako ya kurekebisha kosa weka ratiba ya wakati ambapo tatizo litarekebishwa.

MWISHO KABISA: Chukua hatua za haraka kutekeleza mpango wa kurekebisha kosa lako, mara baada ya kuahidi kufuata kwa kurekebisha, basi hakikisha uifanye kwa wakati unaofaa na uwajulishe wale walioathirika wakati suluhisho limekamilika.

Usiache kutufuatilia kupitia jarida letu la Mwananchi Scoop linalotoka kila Ijumaa kwa habari mbalimbali, makala, afya, burudani na michezo. asantee.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags