Jinsi ya kufanya nywele zako ziwe nyeusi

Jinsi ya kufanya nywele zako ziwe nyeusi

Ooooooh! niaje wanangu sana natumai ni wazima wa afya naona ni furahi day nyingine tena tunakusogezea jarida letu pendwa kabisa, basi bwana leo kwenye kipengele chetu cha fashion tuna mada konki kabisa kuhusiana na suala zima la kufanya nywele zako ziwe nyeusi.

Nywele nzuri ni matunzo na matunzo hayo yanajumuisha routines mbalimbali za kutunza nywele, kama kuosha nywele, kufanya steaming (steaming ya kawaida na protein treatment), kuzipa nywele unyevu.

Hivyo pale kimoja kinapopuuziwa/kukosekana lazima nywele zisikue vizuri  na kutokuwa na rangi nzuri ya kuvutia (NYEUSI), kitu ambacho kinawakera watu wengi sana.

 

Leo tuangalie sababu mbalimbali ambazo zinafanya nywele zisiwe nyeusi na zakuvutia.

 

 • Kutopata mlo kamili na kutokunywa maji ya kutosha
 • Nywele kukosa matunzo stahiki
 • Kutumia bidhaa zisizofaa kwa nywele zako (bidhaa zinatumika kulingana na hair type
 • Msongo wa mawazo
 • Kutumia dawa zenye kemikali kali (Relaxer)Hayo hufanya nywele zako kukosa ule mvuto wake wa asili kabisa na kutopendeza na kuvutia, hivyo kuwakosesha raha watu wengi sana wanaozingatia muonekano mzuri wa nywele zao.

Leo tuangalie procedure nyepesi tu inayoweza kuurudisha muonekano wa nywele zao ndani ya muda mfupi sana, zikawa nyeusi na za kuvutia.

 

MAHITAJI

 • Tui la nazi
 • Mafuta kijiko kimoja (Black Castor oil, Coconut oil or Jojoba oil)

 

JINSI YA KUFANYA ILI NYWELE ZAKO ZIRUDI KATIKA MUONEKANO MZURI

 

 • Chukua nazi iliyokomaa vizuri, kisha ikune kwa utaratibu ili utoe vipande vidogo vidogo na kuifanya iwe laini au unaweza tumia mbuzi au Coconut blender kukwangua nazinyako.
 • Weka maji kidogo na uchuje tui katika chombo kisafi, hakikisha unapata tui la kwanza likiwa zito kabla halijakatika.
 • Osha nywele zako kwa maji safi yenye uvuguvugu mpaka uhakikishe hakuna mafuta wala uchafu ulioganda kwenye ngozi ya kichwa.
 • Baada ya kufuta maji yote kichwani, chukua tui lako la nazi, anza kupaka kwa kuchambua nywele kidogo kidogo hadi uhakikishe zote zimekolea vizuri.
 • Vaa kofia ya plastic au ingia kwenye steamer au mfuko kwa muda wa saa moja kuliacha tui la nazi lifanye kazi vizuri kichwani.
 • Baada ya hapo, osha nywele zako, kausha na upake mafuta mazuri kwa ajili ya nywele.

Fanya  hivi kila week nywele zako  zitaimarika na kuwa na afya kwa haraka zaidi.

Njia hii inaweza kuwa rahisi kuliko zote kutokana na unafuu wake na upatikanaji wa nazi kwa kuwa kila mmoja anaweza kupata.

Haya haya mada yetu leo bwana ilikuwa ni fupi na yenye mafunzo mengi sana, natumai utajaribu ili kuweza kubadirisha muonekano wako wa nywele, watu wengi wanajua nywele mpaka uzaramikie kwa pesa nyingi lakini ni vitu vidogo na vya asili ambavyo vinaweza kukusaidia.

Usiache kufuatilia jarida letu la @Mwananchiscoop kwa kupata habari kedekede za burudani, michezo, fashion na wale wazee wa umbea uko kama woteeeh!.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post