Jinsi ya kuepukana na kunuka mdomo

Jinsi ya kuepukana na kunuka mdomo

Na Aisha Lungato

Niaje wanangu wa mwananchiscoop I hope mko powa leo bwana kwenye fashooon nimekuja na ile tiba ya kutoa harufu mbaya mdomoni waswahili tunasema mdomo unatemaa, ungana na mimi kukomosha tatizo hilo.

Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako.

Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.

Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

Kinacho sababisha harufu mbaya mdomoni


Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula).

Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na madawa (medications) Kuvuta sigara, kunywa kahawa, ulaji wa vyakula vyenye viungo vikali kama vile vitunguu maji au thaumu.

Namna ya kujua kama una harufu mbaya mdomoni


Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).

Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.

Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

Nikwambie tu bado yakomengi ya kujifunza kufuatia tatizo hilo hivyo endelea kufuatilia jarida letu ili uweze kupata maarifa zaidi.

Itaendelea…………………………………..






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags