Jinsi ya kipika Mikate ya Ufuta

Jinsi ya kipika Mikate ya Ufuta

Mambo vipi ni jumanne nyengine tena tunakutana kwenye kipengele cha Nipe dili kama kawa kama dawa leo tutajifunza jinsi ya kupika mikate ya Ufuta.

Je unaifahamu mikate ya ufuta wewe? Hahaha twende sawa hii ndiyo nipe dili bwana hatushindwi jambo. 

Vipimo hivi hapa kwa kuanza ukiwa unahitaji kutoa mikate 6


Unga- 3 Vikombe vikubwa (Mugs) vizuri ukatumia unga wa DAHABI au AL WATAN
Tui la nazi - 2 ½ (Mugs)
Hamira - Vijiko 2 vya supu
Chumvi - nusu kijiko
Sukari - kijiko 1 cha chai
Yai - 1
Ufuta - Kiasi
Mafuta au samli Ya kupakia mkate - Kiasi


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.Changanya pamoja unga, nazi, chumvi, hamira, sukari na yai. 2.Hakikisha unga wote umetoka madonge na umevurugika vizuri uwe laini. (uwe maji maji kama wa kaimati lakini unakuwa mzito kidogo kuliko wa kaimati).
3.Usubiri uumuke (Ufure) 

Jinsi Ya Kuchoma Mikate:

1.Hakikisha chuma cha kuchomea kiwe kinagandisha vizuri (Kisiwe non- stick) na pia kisiwe kilichopikiwa mafuta.

2.Weka chuma kwenye moto, kikipata moto rushia maji ya chumvi kidogo halafu tia unga kiasi kama kiganja kimoja cha mkono

3.Utawanye vizuri kwa vidole halafu nyunyizia ufuta juu yake.
4.Ukianza kuwa mkavu nyanyua chuma kifudikize kwenye moto

mpaka mkate wako uwe rangi ya dhahabu.

5.Toa kwenye chuma kwa kutumia kisu.
6.Paka samli au mafuta juu ya mkate kwa tumia brush.
7.Endelea hivyo hivyo mpaka umalizie unga wote.

Haswaaaa baada ya yote hayo hapo bwana tayari mikate yetu kwa kuliwa unaweza ukala kwa nyama ya kuku, ng’ombe au kutolea na kachori hata katlesi inafaa pia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags