Jezi ya Yanga yapepea kwenye video ya AFCON

Jezi ya Yanga yapepea kwenye video ya AFCON

‘Jezi’ ya ‘klabu’ ya #Yanga imetumika kwenye video ya promo ya michuano ijayo ya mataifa ya Afrika #AFCON, inayotarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast kuanzia January 13 hadi Februari 11 mwakani.

Katika michuano hiyo ambayo inahusisha timu 24 Tanzania pia imefuzu ikiwa ndiyo timu pekee kutoka ukanda CECAFA.

Hii itakuwa ni michuano 34 kufanyika ambapo kwa sasa bingwa mtetezi ni timu ya taifa ya Senegal iliyochukua ubingwa mbele ya Misri.

Mbunifu wa jezi hiyo #SheriaNgowi ameishukuru #Yanga kwa kumpa nafasi ya kubuni ‘jezi’ hiyo hadi ikawekwa kwenye video hiyo akisema kwake ni heshima kubwa.

Ngowi ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ame-post video hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags