Jennifer lopez achumbiwa tena

Jennifer lopez achumbiwa tena

Muigizaji na muimbaji Jennifer Lopez ametangaza kuwa atafunga pingu za maisha baada ya wapenzi hao kusitisha harusi yao.

Lopez mwenye umri wa miaka 52, alidokeza kuwa amechumbiwa kwa mara ya pili na nyota wa Hollywood Affleck katika ujumbe aliyouweka kwenye mtandao wake wa OnTheJLo.

Msanii huyo alisema wale ambao si watu wake wa karibu watalazimika kujiunga na tovuti yake ambapo anaweka maisha yake binafsi ili kupata habari mbalimbali zinazomuhusu.

Hata katika video aliyoposti Lopez ameonekana akilia wakati anavishwa pete ya uchumba na mpenzi wake huyo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags