Jemie: Casemiro Hafai kuwepo Man United

Jemie: Casemiro Hafai kuwepo Man United

Mwana-soka wa zamani wa ‘klabu’ ya Liverpool na Uingereza #JemieCarragher amedai kuwa mchezaji wa Manchester United Casemiro hafai kuwa ‘klabuni’ hapo hivyo anapaswa kuwa kwenye ligi za ushindani kama Saudia na Marekani.

Jemie ametoa kauli hiyo baada ya kiungo huyo kucheza katika kiwango cha chini sana kwenye mchezo wa ‘Ligi’ Kuu ya Uingereza siku ya jana Jumatatu ambapo Man United walipokea kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Crystal Palace.

Siku ya jana mchezaji huyo hakuonesha kiwango kizuri kama ilivyo zoeleka ambapo alipitwa zaidi ya mara saba na kupokonywa mipira na washambuliaji wa #Palace.

Ikumbukwe kuwa Casemiro mwenye umri wa miaka 32 raia wa Brazil aliingia ‘klabuni’ hapo Agosti 22 mwaka 2022 akitokea ‘timu’ ya Real Madrid.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags