Jela kwa kujirekodi anakula popo

Jela kwa kujirekodi anakula popo

Hii imetokea huko nchini  Thailand ambapo Mwanamke mmoja raia wa nchi hiyo aliyefahamika kwa majina , Phonchanok Srisunaklua anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela au faini ya hadi takribani TZS milioni 32.5 baada ya kurekodi video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akila popo.

Mwanamke huyo alirekodi kipande hicho kwenye ukurasa wake wa Facebook, akionesha popo waliokuwa kwenye bakuli la supu na kuanza kuwakunjua mbawa zao kabla ya kuanza kuwala huku akiwaelezea jinsi walivyo na ladha nzuri.

Video hiyo imeleta upinzani mwingi kutoka kwa watumiaji wa mtandao ambao waliibua wasiwasi kuhusu athari za kiafya za vitendo vya Srisunaklua huku mmoja wa madaktari wa mifugo akikemea kitendo hicho kwa kuwa popo wana vimelea vingi vya magonjwa na hakuna uthibitisho kwamba maji ya moto yanaweza kuua vijidudu hivyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags