Na Aisha Charles
Weeeeh! It’s furahidayyyyy! Kama mnavyojua afya ndo jambo la muhimu na msingi sana katika mwili wa mwanadamu, hivyo basi hatuna budi kukusogezea mawili matatu ambayo yatakuelimisha kuhusiana na maswala mazima ya afya yako.
Hivi niwaulize swali kidogo, kila mtu anajua kundi lake la damu? au tunaishi tuu bali maisha yaendee, so kama hujui chakukushauri leo ni kuchukua hatua na kwenda kujua kundi lako la damu hii itakusaidia Zaidi kuliko hata unavyofikiria.
Watafiti wanasema makundi ya damu yanaweza kaendana na tabia yako kwa asilimia kubwa, Mfano hasira, upole, hadi vya kula unavyo tumia kila siku.
Kama tunavyojua kuna zile tabia mtu anarithi kutoka kwa wazazi wake either baba au mama lakini kuna zile ambazo anazaliwa nazo by nature sasa hizi ndo hizo tunazozizungumzia kuwa zinatokana na kundi lako la damu.
Ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua ni kwavipi katika baadhi ya tabia zako zinatokana na kundi lako la damu…
Kwanza kabisa unatakiwa ujue makundi ya damu ambayo ni manne kuna A,B,O na kundi AB kwa kawaida kila binaadam yupo katika kundi moja wapo kati ya makundi hayo manne.
Makundi hayo yana weza kutumika kujua tabia za binadamu na hii yaweza kuwa rahisi kujua tabia ya mwanaadamu bila kutumia nyota au njie nyengine nyingi kama ambavyo wengi wanafanya kupitia wataalamu mbalimbali.
Wataalamu wanasema tabia na kundi la damu ina uhusiano mkubwa tofauti na vyanzo vyengine ukweli nikwamba yana weza kutuonyesha vile mtu ana vependelea na asivyo pendelea kazi anazo pendelea ,watu anaopendelea kujiunga nao katika jamii na hata katika upande wa vyakula kuna vyakula haviruhusiwi kula watu wa kundi fulani.
Hata hivyo baadhi ya watafiti nchini korea wame bainisha kuwa hata unavyo pendelea kukaa yaani mtindo wakukaa.
Kundi lako la damu linaweza kukufanya uwe dhaifu au imara yote hayo yanawezekana kabisaa au linaweza kukufanya usiuguwe baadhi yamagonjwa Fulani nafikiri hii kila mtu kashawahi isikia.
- Kundi ‘A’ la damu
Watu wakundi hili la damu huwa ni mfano wakuigwa wapiganaji sikuzote hawa watu niwenye mafanikio tu, ni watu wema wapole na wenye tabia njema pamoja na hayo ni rahisi sana watu waainahii kupata msongo wa mawazo kwasababu hupendelea kufikiri vitu vikibwa mno.
Kundi A pia wanapenda vitu vyao vikamilike kwa hali ya juu yaani huwa wanapenda mambo yalionyooka na sio ubabaifu na wanaweza kuchambua mambo sawia bila kusahau ni waaminifu sana.
Wanahisia kali hata kwenye vitu vya kawaida mfano kushabikia mpira hapa watu wenye group A mbona mtaminyana, so unaweza kuangalia hapa kundi lako hilo A hatakama huna tabia zote hizi lakini lazima kuna baadhi utakuwa unazo.
Mapundufu ya watu wa kundi ‘A’ ya damu
Wasumbufu, wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida wakitaka kitu ametaka yaani hii huwezi pingana nae, waswahili husema akitaka lake lazima alipate. wanaibu, wengine wa kimya zaidi na wana penda kujichanganya na watu bila kujali mazingira au jamii.
Niwatu wa gharama sana hasa wadada au wanawake hupendelea vitu ambavyo vipo njee ya uwezo wao.
Kwenye maisha ya kijamii
Nimtu ambae unaweza kumuaamini na kumtegemea katika majukumu wanapenda ufanisi wakiwango cha juu sana.
Wote huepuka shari misuguano na magomvi pia mara nyingi hawapendezwi wala kufurahishwa na sherehe zenye makelele (sehemu yenye kelele) wanapendele ukimya na utulivu.
Watu wa kundi ‘A’ la damu kazini
Unaweza kumuamini na kumtegemea katika majukumu, wanapenda ufanisi wakiwango cha juu, bahati mbaya au nzuri sijui tuseme hivyo wanajaili sana hata vitu vidogo mfano hata ukimpa zawadi ya pen ataithamini daima.
Ngumu sana kuwaelewa mtindo wao wa maisha tunaweza kusema niwasiri sana, wasio waelewa vyema watu wa kundi hili wana weza kupata shida kwasababu ni waaminifu sana mara nyingi wanapekuwa watumishi au maafisa wa taasisi..
KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI KUNDI A LA DAMU
Ningumu sana kwa kufunguka hasa pale linapotea swala kumwambia mtu ana mpenda na kushirikisha mambo yao hivyo basi ukitaka kuchumbia watu wa kundi A la damu uwe na uvumilivu.
Lakini wakiamua kupenda utawafahamu wakati wowote huwa wanapenda kweli, wana penda kujificha kama ni usiku hukaa gizani.
Ukweli nikwamba watu wa kundi A la damu ni wa bunifu kingine cha kumalizia katika kundi A ni watu amabao wanalewa sana hata kama kilevi ni kidogo, walevi wenyewe wanawaitaka vichwa panzi. Hata hivyo hupendelea kula mboga za majani na matunda ya sio kuwa na acid.
Eeeeh! Siwanasemaga mdogo mdogo ndo mwendo basi nasisi leo hatuna budi kuishia hapa kwa kuhofia kukuchosha msomaji wetu, sisi tunataka kukuelimisha wewe kwa namna ya pekee sana. Usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop kwaajili ya kujifunza Zaidi.
ITAENDELEAAA…
Leave a Reply