Jay Z amaliza utata wa swali alilolitoa

Jay Z amaliza utata wa swali alilolitoa

Baada ya kuuliza swali kwa mashabiki kuwa kupata chakula cha usiku na Jay Z au akupe dola 500 ambayo ni sawa na zaidi ya billion 1 za kitanzania, utachaguwa nini, Jay amemaliza utata huo kwa kutoa ushauri kwa mashabiki zake kuwa ni bora wachukue pesa hizo.

Kupitia mahojiano yake na #CBcMorning Jay amewajibu mashabiki ambao wanaamini kupata chakula cha jioni na msanii huyo watapata maarifa ambayo yatakuwa na faida kwao huku wakiamini kutengeneza fedha nyingi zaidi ya hata hiyo Billion 1.1.

‘Rapa’ huyo amewashauri kwa kusema kuna ni bora kuchukua kiasi hicho cha fedha na ununue ‘albam’ zake kwani utapata maarifa ya kutosha kwasababu kila kitu amekiimba kwenye ngoma zake kuliko kupata chakula cha usiku na yeye.

Huku akiweka wazi kuwa hata angekuwa yeye angechagua pesa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags