Japani yatoa mafunzo ya kucheka

Japani yatoa mafunzo ya kucheka

Watu wengi nchini Japani wameanza kuchukua mafunzo ya jinsi ya kutabasamu upya baada yakuvaa mask (Barakoa) kwa muda mrefu.

Raia hao wamekua wakizoea kuvaa mask kwa muda mrefu jambo lililopelekea wengi wao kusahau kabisa jinsi ya kutabasamu, somo la kutabasamu linafanywa kwa msaada wa vioo vya mikononi.

Masomo ya kutabasamu nchini humo yanazidi kua maarufu kwani yanaongeza ukaribu wa mawasiliano na ustawi na afya.

Sambamba na hayo mwalimu wa tabasamu, Keiko Kawano amedai kuwa watu hawakucheka kwa muda mrefu wakiwa chini ya barakoa na wanakabiliana na changamoto.

“Watu hawajainua mashavu yao chini ya barakoa au kujaribu kucheka sana sasa, wako katika wakati mgumu”alisema Kawano.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags