Japan yazindua intaneti ya 6G

Japan yazindua intaneti ya 6G

Makampuni ya mawasiliano ya simu nchini Japan, DOCOMO, NTT Corporation, NEC Corporation, na Fujitsu yamezindua kifaa cha kwanza cha 6G dunaini ambacho hutoa kasi ya utumiaji data mara 20 zaidi ya mitandao ya sasa 5G.

Kuanzishwa kwa kifaa hiki cha kisasa kunaiweka Japan katika mstari wa mbele katika mbio za kimataifa za kuendeleza na kusambaza mitandao ya simu ya kizazi kijacho.

Hata hivyo, hatua hii ya kuingia kwenye teknolojia hii mpya inahitaji miundombinu mipya, huku ikielezwa kuwa huenda ikapita muda kidogo kabla ya 6G kuweza kutumika kwa umma.

Kwa sasa takribani dunia nzima watu hutumia Intaneti ya 5G ambayo ilianza kutoa huduma rasmi 1 Oktoba 2018.

 

Yapi maoni yako kuelekea kasi ya 6G?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags