Jackie Chan atolea ufafanuzi picha yake

Jackie Chan atolea ufafanuzi picha yake

Ikiwa zimepita wiki kadhaa tangu picha ya mwigizaji kutoka China, Jackie Chan kuzua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana akiwa ameota mvi kichwani na kwenye ndevu, sasa mwigizaji huyo ametolea ufafanuzi picha hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jackie amewatoa hofu mashabiki kwa kueleza kuwa hana tatizo lolote la kiafya bali picha hizo ni kwa ajili ya kazi yake mpya inayotarajia kutoka hivi karibuni.

Katika maelezo yake amedai kuwa uhusika anaotakiwa kucheza katika kazi hiyo mpya anatakiwa kuwa na muonekano wa mtu ambaye anamvi kichwani na kwenye ndevu.

Kwa sasa Jackie Chan ana umri wa miaka 69, alizaliwa mwaka 1954 Victoria Peak, Hong Kong. Alianza kucheza katika filamu maarufu ya 'Bruce Lee Enter the Dragon' na baadaye akawa msanii mkubwa aliwahi kutunukiwa tuzo ya heshima ya Oscar mnamo 2016.

Jackie Chan anajulikana zaidi kupitia filamu zake kama ‘Ride on’, ‘Twinkle, Twinkle, Lucky Stars’, ‘The Twins Effect’, ‘The Karate Kid’, ‘The Foreigner’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags