Irine Uwoya kuingia kwenye Ndoa

Irine Uwoya kuingia kwenye Ndoa

Alaaah! Kutoka ukurasa wa Instagram wa Muigizaji wa bongo movie Irene Uwoya mapema ameweka ujumbe huu mtandaoni ulioibua wadau mbalimbali ikiwemo wasanii wenzake kumtakia heri.

Sasa bwana ujumbe alioandika ni huu hapa "I can’t wait for my wedding
I love you krish 
" Maneno hayo ambayo ameyaandika yakiwa na maana kuwa yupo tayari kwa ajili ya kuingia kwenye ndoa siku za hivi karibuni.

Baada ya kuandika ujumbe huo uliyoambatana na picha zake pamoja na mtoto wake Krish uwanja wa comment wasanii mbalimbali walifunga na kumtakia kila la kheri akiwemo Wema Sepetu, Auntyezekiel, Mc  Garab na wengine.


Hata hivyo nikukumbushe tu kwamba haitakuwa ndoa yake ya kwanza kufunga Msanii huyo ikiwa ni miaka kadhaa imepita tangu alipofunga ndoa na msanii wa bongo fleva dogo Janja  na haikudumu.

Aisee ni kweli mrembo huyo anaingia kwenye ndoa au kama kawaida yao kiki? Dondosha comment yako hapo chini kupitia www.mwananchiscoop.co.tz






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags