Inter Milan watwaa taji la 20 serie A

Inter Milan watwaa taji la 20 serie A

'Klabu' ya Inter Milan imecheza ‘soka’ la kibabe ikiichapa mahasimu wao AC Milan mabao 2-1 na kutwaa taji lao la 20 la Serie A huku ikiwa bado na ‘mechi’ tano mkononi.

Staa Francesco Acerbi alitumia uzembe wa mabeki wa AC Milan kuifungia Nerazzurri bao la mapema ndani ya dakika 20 za mchezo. Na baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga, Inter ilifunga bao la pili, shukrani kwa kazi nzuri kabisa ya Mfaransa, Marcus Thuram kwenye dakika ya 49.

Fikayo Tomori aliifungia AC Milan bao la kujifariji dakika za mwisho kabla ya vuta nikuvute iliyotokea mwishoni iliyowahusisha mastaa Theo Hernandez, Denzel Dumfries na Davide Calabria na wote walionyeshwa kadi nyekundu.

Lakini, mwisho wa ‘mechi’, Inter ndiyo iliyopata ushindi dhidi ya mahasimu wao hao na kunyakua taji lao la kwanza la Scudetto tangu msimu wa 2020-21.

Kwa Simone Inzaghi, alisherehekea taji lake la kwanza la Serie A akiwa kocha, akiongeza pale kwenye mataji matatu ya Coppa Italia na matano ya Italian Super Cup ambayo amebeba katika kipindi chake cha ukocha..
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags