Ingiza sh.10,000 kila siku kwa biashara ya mishikaki

Ingiza sh.10,000 kila siku kwa biashara ya mishikaki

Safari ya mtu yoyote yule katika biashara na ujasiriamali haijakuwa rahisi. Hii ni kwa sababu hakuna nafasi inayokuja kwa urahisi haswa kwa wanawake.

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa ilitoa ripoti yake inayoonyesha ongezeko maradufu la thamani ya biashara ya bidhaa zitokanazo na ubunifu kutoka dola bilioni 208 mwaka 2002 hadi dola bilioni 509 mwaka 2015.

Ripoti hiyo ambayo ilikuwa toleo la pili la tathmini ya uchumi utokanao na bidhaa za ubunifu ilizinduliwa huko Geneva, Uswisi ambapo UNCTAD ilisema kuwa China ndio inaongoza kwa kiasi kikubwa katika biashara hiyo ya bidhaa za ubunifu inayohusisha ubunifu wa majengo, mitindo ya mavazi na maonesho, usanifu wa ndani ya nyumba na hata sanaa za filamu na vikaragosi.

Akizungumza na wanahabari mjini Geneva wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Mkurugenzi wa kitengo cha biashara ya kimataifa na bidhaa UNCTAD, Pamela Coke-Hamilton alisema takwimu hizi ni muhimu kwa namna mbili, “uchumi wa kiubunifu una utajiri wa kibiashara na pia kiutamaduni.

Thamani hizi mbili zinasababisha serikali duniani kote kujikita katika kukuza na kuendeleza uchumi wa kiubunifu kama sehemu ya mikakati ya mabadiliko ya kiuchumi na juhudi za kuhamasisha mafanikio na maisha bora.

Kwa kupitia ripoti hii tunaona wazi kuwa biashara za ubunifu zinaweza kukua zaidi na kumfanya mtu kupata kipato cha kutosha kuendesha maisha yake.

Ukipita sasa hivi maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam utaona jinsi vijana walivyojiajili kwa kuuza mishikaki pamoja na ndizi.

Vijana hao wamekuwa wakitembeza katika maduka na watu wa njiani hivyo kujipatia riziki zao za kila siku.

Nami leo nakujuza kuwa ni kweli biashara ya mshikaki inaweza kukupatia faida ya Sh. 10,000 kila siku ukiamua kuifanya kwa uwaminifu mkubwa.

Mahali pa kufanyia biashara ni eneo lolote lenye watu wengi na hauhitaji fremu, mahali hapo panaweza kuwa jirani na soko, maeneo ya kituo cha mabasi, shuleni, vyuoni, ufukweni au eneo lenye wapitaji wengi.

Ujuzi

Ujuzi unaotakiwa ni kuchoma mishikaki mitamu kwa kuchanganya viungo vyote vinavyohitajika pamoja na jinsi ya kukata vyama vipande na bei yako(500 inafaa sana kwa kuanzia)

Kama huna ujuzi usiogope tembea youtube kuna mafunzo mengi ya kutengeneza mishikaki mitamu na viungo vyote vinavyohitajika.

Mahitaji

Tatufa jiko (Nenda sehemu wanapochomelea unaweza kuongea nao vizuri jiko linapatikana ukiwa na 23000Tsh).

Pata nyama isiyo na mifupa (Steki Kwa kuanza na kilo 2 Bei ya kilo ni 8000Tsh maeneo mengi).

Mkaa (Kupo tatu ni 1500Tsh).

Viungo vyote vinavyohitajika (Makadirio ni 5000).

Vijiti vya mishikaki (2500Tsh).

Kwenye 2kg unaweza pata faida ya 10,000Tsh baada ya kutoa matumizi yako vyote.

Na biashara umeanza kwa mtaji wa 23000+8000X2+1500+5000+2500=48000 tu.

Note:Ukataji wa vipande unahakisi faida, mfano tuseme ili upate faida ya 10000Tsh lazima upige hesabu.

Hesabu ya kulenga faida kwenye mishikaki ipo kwenye vipande, sasa ili kujua vipande unavyotakiwa kukata:

    vipande=(mtaji+faida unayolenga)/(bei ya kipande)

  mfano kwa kilo 2(mtaji=48,000, faida nayolenga ni 10,000 kipande nauza 200)

 vipande = (48,000+10,000)/200

 vipande = 290

Kwa hivyo ili kupata faida ya 10,000 kwenye 2kg ya steki natakiwa nikate vipange 290.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags