Indonesia yapiga marufuku dawa za maji kwa watoto

Indonesia yapiga marufuku dawa za maji kwa watoto

Indonesia imepiga marufuku kwa muda dawa zote za maji kufuatia vifo vya watoto wapatao 100 kutokana na uharibifu wa figo. Haya yameripotiwa leo na wizara ya afya nchini humo.

Wizara hiyo imesema kwamba takriban visa 206 vya uharibifu mkubwa wa figo vimeripotiwa katika mikoa 20 tangu mwezi Januari na idadi hiyo imeongezeka kwa kasi tangu mwezi Agosti. Waziri wa afya Budi Gunadi Sadikin, amesema idadi halisi ya visa hivyo huenda ikawa juu na kiwango cha vifo cha karibu 50%.

Sadikin amesema wizara hiyo imefanya uchunguzi na kubaini kuwa watoto walioathirika kutokana na jeraha kubwa la figo walikuwa wametumia kemikali tatu hatari ambazo ni - ethylene glycol, diethylene glycol na ethylene glycol butyl ether. Wizara hiyo imesema visa vingi vilihusisha zaidi watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags