Indonesia, watu sita wamefariki baada ya mlipuko uliotokea mgodini

Indonesia, watu sita wamefariki baada ya mlipuko uliotokea mgodini

Watu 6 nchini Indonesia wamekufa na wengine wawili wamejeruhiwa leo baada ya mlipuko uliyosababishwa na gesi kwenye mgodi wa makaa ya mawe Magharibi mwa Indonesia katika mkoa wa Sumatra.

Rumainur ambaye ni afisa katika wakala wa ulinzi wa raia wa mkoa huo amesema watu watano walifanikiwa kuondoka katika shimo la mgodi huo wa wilaya ya Suwahlunto baada ya mlipuko huo, huku wawili kati yao wakiwa na majeraha mabaya yatokanayo na moto.

Aidha msemaji wa polisi wa mkoa, Dwi Sulistiawan, amesema kumekuwa na ajali kama hizi katika eneo hilo, hasa kutokana na chembechembe za vumbi ya makaa ya mawe kugusana na vyanzo vya joto.

Mji wa Sawahlunto ulijengwa na wakoloni wa Uholanzi katika karne ya 19 kama mji wa uzalishaji wa makaa ya mawe.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags