Imam aliyerukiwa na paka akiswalisha apewa Tuzo

Imam aliyerukiwa na paka akiswalisha apewa Tuzo

Imam Walid Mahsas kutoka nchini Algeria, alietrend kupitia mitandao ya kijamii ambapo clip yake ilimuonesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tuzo hiyo amabayo ametunukiwa na Serikali ya Algeria chini ya Ofisi ya masuala ya dini kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu unazingatia huruma na Upendo kwa wanyama.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia nyingi kutoka kwa watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kuwa imara kwa kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala.

Jambo la kujifunza katika hili, kitu chochote unachokiona kidogo lakini kwenye macho ya watu wengine nikikubwa mno, tusiache kutenda mema, haya mtu wangu wa nguvu dondosha komenti yako hapo chini kutujuza mtazamo na maoni wako katika hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags