Ijue sheria juu ya haki na wajibu wa wafanyakazi wa kazi za ndani

Ijue sheria juu ya haki na wajibu wa wafanyakazi wa kazi za ndani

Ama kweli mambo ni mengi muda ni mchache, ni wiki nyingine tena tunakutana hapa kwenye segment ya kazi chimbo pekee tunakusogezea mambo mbalimbali kuhusiana na ajira.

Na leo nimeamua nilete jambo muhimu si mnajua siyo kila siku tuzungumzie watu wanaotulia kwenye viyoyozi lazima na hawa wenzetu wengine tuwakumbuke, wadada wa kazi ni watu ambao ukiishi nao kwa upendo nao huonesha upendo lakini ukiishi nao vibaya basi na wewe utegemee ubaya.

Matukio ya wafanyakazi wa ndani kutokupewa mishahara yao na kufanya mambo mabaya kwa watoto wa ‘mabosi’ zao imekuwa ni suala ambalo haliepukiki ambapo mpaka sasa baadhi ya watu hawataki kabisa wafanyakazi wa kazi za ndani majumbani mwao.

Nipo hapa kuzungumza na wewe mfanyakazi ambaye unapitia changamoto fulani suluhisho siyo kufanya matendo mabaya bali nikufuata na kujua sharia yenu, na leo niko hapa kueleza sheria itakayo kusaidia kupata haki yako.

Sheria ya kazi ya Tanzania ( EMPLOYEMENT AND LABOUR RELATION ACT  Cap 366 R.E 2019 AND LABOUR INSTITUTIONS ACT Cap 300 R.E 2019 ) 

zimeelezea haki na wajibu wa mfanyakazi na mwajiri pahala pa kazi kwa kuonesha vifungu vya sheria kulingana na sekta husika au eneo la kazi.

Mfanyakazi wa kazi za ndani  ni mtu yeyote anayefanya kazi za nyumbani kama kutunza mifugo, usafi wa nyumba, kufua, kupika au kulea watoto na kupewa ujira/mshahara mwisho wa mwezi au kwa siku inategemea na makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Sheria ya kazi ya Tanzania inawalinda pia wafanyakazi wa kazi za ndani (domestic workers ) kama walivyo wafanyakazi wengine ingawa sheria haijataja specific haki au wajibu wa mwajiri /mwajiriwa wa kazi za ndani.

Tanzania ni miongoni mwa wanachama wa Shirika la kazi Duniani (ILO) hivyo ni lazima kupitisha makubaliano (Convention and Recommendation) katika kulinda haki za wafanyakazi pahali pakazi.

Kupitia mkataba (Convention no 189,  Domestic workers convention of 2011)  imeelezea kiundani haki na wajibu wa mfanyakazi wa kazi za ndani kwanza kabisa kuonesha  umri sahihi wa mtu kufanya kazi kuanzia miaka 18  hata chini ya miaka 18 sheria ina mruhusu kufanya kazi nyepesi pasipo kuathiri afya ya mtoto endapo mwajiri ataenda kinyume na kifungu cha sheria kinavyosema kifungu cha 5(1)&(2) cha sheria ya ajira na uhusiano kazini (ELRA Cap 366 R,E 2019).

Mfanyakazi wa kazi za ndani anahitajika kupewa mkataba wa kazi unaonesha ukomo wake wa kazi, jina la mwajiri, aina za kazi anazostahiri kufanya,  kiwango cha mshahara imeelezewa zaidi kifungu cha 13 na 14 cha Sheria ya ajira na uhusiano kazini (ELRA Cap 366 R,E 2019) iko sambamba na kifungu cha 7 cha mkataba wa kimataifa wa 2011 (domestic workers conv no 189 of 2011)

Licha ya haki za wafanyakazi wa kazi za ndani pia wana wajibu wao katika eneo la kazi kama kuheshimu na kuipenda kazi yake, kutunza siri za mwajiri, kumuheshimu mwajiri wake na familia kiujumla.

Wafanyakazi wa kazi za ndani na wafanyakazi wengine wanalindwa na sheria kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria za kimataifa, ”Tambua sheria utende haki na kuzingatia wajibu kulingana na nafasi uliyonayo katika eneo la kazi, kisha fuata sheria”.

Kwa leo mimi naishia hapa i hope tumeelewana japo tumeandika kisheria zaidi hatukua na jinsi sisi lengo letu ni wewe mpendwa wetu uweze kujua sheria inayohusu mahala pa kazi, sina la ziada tukutane tena wiki ijayooooooooh.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post