Ijue aleji ya chakula na inavyotokea

Ijue aleji ya chakula na inavyotokea

Na Aisha Lungato

Tatizo la aleji au mzio ni kubwa na mara nyingi husababisha vifo kwa waathirika.

Mpaka sasa bado hakuna dawa ya kutibu mzio au aleji lakini kuna dawa za kupunguza na kutibu madhara ya aleji na kupunguza tatizo.

Dawa hizi hupunguza mpambano kati ya kinga ya mwili na kitu kilichoingia ndani ya mwili ambacho hukusababishia mzio. Habari njema ni kwamba kuna vyakula asili na virutubisho ambavyo vinaweza kutumika kutibu aleji kwa kiasi kikikubwa sana.

Mratibu wa Lishe Manispaa ya Temeke Dk. Charles Malale anafunguka na kueleza kwa kin aleji ya chakula inatokeaje.

Alisema ndani ya seli za mwili kuna kemikali zinazoitwa histamine, kazi yake ni kuiruhusu kinga ya mwili kupambana na kitu chochote kigeni ambacho kimeleta athari kwenye tishu zako.

Dk. Malale alisema kinga ya mwili inaweza kupambana na kitu chochote ambacho kinaleta shida kwenye mwili mfano vimelea vya ugonjwa, hewa chafu, virusi, bacteria, baadhi ya vyakula.

“Kwahiyo tunaelewa sasa kwamba histamine husababisha aleji juu ya chakula fulani. Maana yake umekula lakini mwili unaonesha kukikataa chakula hicho kwasababu mwili umeona kinaweza kuleta madhara makubwa.

“Kemikali hii ya histamine ndio inaleta matokeo kama kutapika, kukohoa au kujikuna. Hivyo basi unapotumia mara nyingine kitu au chakula husika mwili utakumbuka kwamba kiliwahi kuleta madhara ndipo haitaruusu kiingine ndani ya mwili tena,” alisema

Dalili za kuwa umepata aleji

Alisema viashiria kwamba una aleji ya chakula hujionesha mapema zaidi, ndani ya dakika au masaa kadhaa baada ya kula chakula husika.

Dk. Malale lisema moja ya dalili hizo ni kutokwa na malengelenge yanayowasha kweye ngozi, mdomo kuvimba, kutetemeka na kuwasha, ulimi kuvimba, koo na uso, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo.

Alisema dalili zingine ni kukohoa sana na mafua makali, mwili kuchoka sana na kujiskia uvivu, kupata ugumu kupumua ama pumzi kukata pamoja na kupoteza fahamu

Hata hivyo Dk. Malale alisema wakati mwingine ni vigumu sana kwa madaktari kugundua chanzo cha aleji ya mtu na hiyo utokana na kwamba kuna vitu viwili, aleji ya chakula na mwili kutovumilia uwepo wa chakula fulani.

Alisema mwili kutovumilia chakula fulani ni kwa sababu aina ya chakula haiwezi kumng’enywa na mwili, mfano kwa watu wengi miili yao haiwezi kumeng’enya vyakula vya ngano na maziwa, vyakula vilivyoongezwa ladha na rangi .

“Watu wanaopata aleji juu ya chakula fulani ni muhimu kuacha kutumia aina hiyo ya chakula mapema iwezekanavyo. Baadhi ya madhara ya kiafya ambayo mtu mwenye aleji na chakula anaweza kuyapata kama tatizo litakuwa ni la muda mrefu ni kama.

“Kupata maumivu ya viungo yasioisha, tatizo l pumu, upungufu wa virutubisho kwenye mwili, tatizo la pumu, upungufu wa virutubisho kwenye mwili, magonjwa ya ngozi, magonjwa yanayotokana na mpambano kati ya kinga ya mwili na tishu za mwili, matatizo ya kumbukumbu, kukosa usingizi pamoja na kuongezeka uzito,” alisema

Alisema kutokana na kwamba aleji ya chakula inaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya anashauri watu kuepuka kula vyakula vilivyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye vifungashio visiharibike.

“Vyakula vilivyosindikwa vimeongezwa kemikali, rangi na ladha vitu ambavyo vinaweza kusababisha aleji na mwili kushindwa kuvimeng’enya. Kwahivo ni muhimu sana kwa mtu mwenye aleji kuwa makini na uchaguzi wa vyakula na vinywaji vya kutumia ili kupunguza athari ya tatizo,” alisema

Aidha alisema utafiti unaonesha kwamba watu wengi wenye matatizo kwenye mfumo wa chakula na matatizo ya aleji hupata nafuu kubwa na afya zao kuimarika pale wanapoacha kutumia vyakula vya ngano.

Alisema tafiiti pia zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya watu wazima wamelalamika kuhusu kuongezeka kwa dalili mbaya za mzio/laji pale wanapotumia vyakula vya ngano.

“Hivyo tunashauri watu wenye mattaizo ya aleji kuacha matumizi ya vyakula vya ngano mara kwa mara,” alisema

Vyakula vya kula kwa mtu mwenye aleji

Alisema mtu mwenye tatizo la kupata aleji anashauriwa kutumia  kwa wingi vyakula kama mbogamboga za kijani.

“Mboga hizi ni kama spinach ambazo zinakuwa na vitamin, madini, viondoa sumu, na viambata ambavyo husaidia umeng’enyaji wa chakua kwa wingi sana. Hakikisha unaongeza mbogamboga za kijani kwenye mlo wako zitasaidia kuimarisha kinga na kutoa sumu mwilini,” alisema

Pia wanaweza kutumia maziwa ya nazi na nazi kwa ni mbadala mzuri wa maziwa ya ng’ombe hivyo maziwa hayo kwa lugha rahisi ni tui la nazi mtu anaweza kutengeneza nyumbani kwake na akaongeza viungo kama limau na tangawizi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags