Ifahamu siri ya msitu wenye umbo la gitaa

Ifahamu siri ya msitu wenye umbo la gitaa

Mkulima mmoja kutoka nchini Argentina, Pedro Martin aliamua kumuenzi marehemu mkewe aliyefahamika kwa jina la Graciela kwa kutengeneza umbo la Gitaa kwa kutumia miti ili mkewe aweze kuliona kutoka mbinguni.

Kwakuwa mke wa Pedro alikuwa ni mpenzi wa Gitaa yeye pamoja na watoto wake wanne walianza zoezi la kupanda miti tofauti tofauti ikiwemo Mikaratusi na Misonobari zaidi ya 7,000 ambayo ilichukua eneo la maili 2/3.

Msitu huo wa Kihistoria upo ‘Pampas’ nchini Argentina na ili uweze kufanikiwa kuona umbo la Gitaa hilo ni lazima upande Ndege au urushe ‘kamera’ ya drones.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags