Ifahamu sheria ya Marekani inayomkataza mwanaume kununua pombe bila kibali cha mkewe

Ifahamu sheria ya Marekani inayomkataza mwanaume kununua pombe bila kibali cha mkewe

Kila nchi au eneo huwa na sheria na kanuni zake ambazo husimamia watu wa eneo hilo, pia katika maeneo mbalimbali duniani kumekuwa na sheria zake juu ya unywaji na uuzaji wa  pombe, “kama vile hairuhusiwi kuuzwa wala kutumia kwa watu walio chini ya miaka 18”.

Fahamu kuwa kwenye Jimbo la Pennsylvania, linalopatikana mashariki ya kati ya Marekani kuna sheria ya pombe ambayo inaeleza kuwa mwanaume haruhusiwi kununua pombe bila ruhusa ya mkewe.

Sheria hiyo inataka ili mwanaume aweze kuuziwa pombe basi anatakiwa awe na ushahidi wa ruhusa ya maandishi kutoka kwa mke wake, maandishi hayo yanatakiwa kueleza kuwa mwanaume huyo ameruhusiwa kununua pombe na mkewe.

Japo kuwa sheria hiyo ni ya  kwenye makaratasi tu kwani haitekelezwi, wanaume wananunua pombe kama kawaida bila ruhusa na hawashitakiwi na wake zao, lakini imekuwa ni kati ya sheria zinazopingwa, wengi wanataka iondolewe kwenye vitabu kwa kufutwa kabisa.

Pia Pennsylvania kama ilivyo katika nchi nyingi watoto hawaruhusiwi kuuziwa vilevi, hivyo basi pombe huanza kuuzwa kwa watu wenye umri kuanzia miaka 21.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags