Ifahamu mitindo ya Afro inayobamba

Ifahamu mitindo ya Afro inayobamba

Aisha Charles

Hii ni special kwa ajili yako wewe msomaji wa magazine ya Mwananchi Scoop kama kawaida tumekutana tena katika segment ya Fashion ili kuweza kujua yale ambayo yatakufanya uwe na muonekano wa kijanja.

Leo tutazungumzia mitindo ya nywele za Afro inayobamba zaidi siku za hivi karibuni. Nikusihi uendelee kusoma kwa ajilii ya manufaa ya urembo wako na kwenda na wakati .

Kwanza kabisa unatakiwa utambue kuwa wewe kijana unataka kuwa mrembo,  katika miaka ya 1960’s hair style ya Afro ilikuwa ni ishara ya kujikubali kwa watu wenye ngozi nyeusi hapa nawazungumzia Waafrika kutokana na nywele zao kuwa tofauti na mataifa mengine, basi walikuwa wanaweka nywele zao za asili kwa mtindo wa Afro.

Watumbuizaji mashuhuri kama Diana Ross na Pam Grier, pamoja na wanaharakati wa kisiasa kama Angela Davis, walikuwa wawakilishi wa harakati hii mpya katika utamaduni na siasa maarufu  huko Marekani hivyo style hii ya nywele waliipitisha kisheria kuingia katika fashion.

Pia miaka ya nyuma vijana wengi wa kike na wa kiume walikuwa wanapenda sana mtindo huu wa nywele, ilikuwa hauwezi kupita njiani bila kumkosa kijana akiwa amechana nywele kwa mtindo wa afro na kuonekana smart, hivyo fashion ya Afro ni ya muda mrefu na isiyochuja lakini kutokana na utandawazi sasa hivi imeboreshwa katika style tofauti.

*Puff Sleek Afro

Hii huwa ni Afro ambazo nywele zake huwa laini na zinakuwa zimejaa sana kichwa kizima ni maridadi na yakuvutia sana ila tu ikumbukwe kwa sasa kulingana na utandawazi siyo lazima nywele zako mwenyewe ukazifanya Afro ila kuna zilizotengenezwa tayari kwa kuvaliwa.

*Double Afro Puffs

Hii unaweza ukaitengeneza mara mbili kama mabutu aidha unaweza ukaanza kusuka kidogo chini halafu juu ukabana Afro mabutu mawili ili kuleta muonekano mzuri.

*Cornrow Afro (Afro ya nyuma yenye mikunjo midogo)

Hii pia unaanza kusuka nywele zako ndogo zenye mvuto chini halafu nyuma ya kisogo ndiyo unaweza kutengeneza Afro nyembamba au ukapachika kibanio ambacho kimetengenezwa Afro za namna hiyo.

Na wembamba wa mikunjo yake huwa inayorudi moja kwa moja nyuma na chini kando ya kichwa chako.

 Oversized (Afro kubwa)

Hii Afro huwa kubwa zaidi kulingana na mtu mwenyewe anavyotaka, ili iweze kupendeza vizuri kwa sababu ni over size unaweza ukainakshia na vibanio ili upate muonekano muziri wenye kupendeza.

Mara nyingi style hii upendelea kuonekana na watu maarufu wakiwa katika mionekano tofauti katika jamii ama kwenye maonesho mbalimbali ya fashion ni nzuri kama utatambua umuhimu wa style mbalimbali katika fashion.

*Picked to Perfection Afro

Hii ndiyo style pekee ya Afro ambayo ilikuwa inatumika miaka ya nyuma na wala haina mambo mengi kwa sababu haiitaji kusuka hata kidogo huenea kichwa kizima na huwa ndefu kwenda juu.

Mwanamitindo na mwanaharakati katika masuala ya jamii kutoka nchini Marekani Ebonee Davis ndiyo mtindo wake pendwa kabisa na humfanya kuwa na muonekano mzuri.

Ila muonekano huu utahitaji ku-shape nywele kulingana na kichwa chako ili uweze kuonekana kwa umbo fulani hivi la duara.

* Small and Mighty Afro (Afro ndogo)

Huu mtindo huwapendeza watu wenye vichwa vidogo kwa sababu zinakuwa Afro ndogo ambazo unaweza kutengeneza kwa kutumia nywele yako ya asili.

Muigizaji mwenye urai wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong'o mara nyingi mtindo wa aina hii hupendelea na unampa muonekano mzuri na huwa anaubadilisha kwa namna ya tofauti. 

 *Coiled Afro (Iliyoviringishwa)

Hii ni Afro iliyoviringisha mithili ya rafu dread lakini yenyewe huwa na mtindo wa kipekee na wengine hupenda kunakishia na rangi tofauti tofauti ili kuwa na muonekano wa kisasa

*Shaped Up

Style hii huwa haina umbo maalumu waweza sema ni rafu iliyokuwa ndefu. Pia kama haujaizoea hii style mara ya kwanza muonekano huo hautauelewa lakini ni mtindo ambao unakwenda na wakati katika soko la fashion

*Bleached Afro

Siku hizi watu katika fashion wamekuwa wakiipenda hii style ya Afro za bleach ambazo zinawafanya kuwa na mionekano mizuri na kwenda na wakati pia.

Ila kuna baadhi ya watu bado wanaona ni style ya kipekee sana na inachagua muonekano wa mtu hapa tunazungumzia rangi ya ngozi ya mtu husika, hata hivyo kunawale ambao hawapendi nywele zao kuweka bleach.

*Afro Bun (Afro za kubana)

Hii style ni nzuri sana kwa sababu haikupi shida unaweza ukabana nywele zako za Afro kama kidoti au mchicha na ukawa na muonekano mzuri wenye kuvutia.

Pia haichagui rangi ya mtu na hata kama ukiwa na kichwa kidogo au kikubwa hii style inaenda vizuri mara nyingi inaweza ikatumiwa na wafanyakazi wa ofisini kwa sababu kuna baadhi ya ofisi hawapendelei kuwa na muonekano uliopitiliza ambao hauko rasmi kwa ofisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post