Ifahamu kazi ngumu zaidi Ufaransa

Ifahamu kazi ngumu zaidi Ufaransa

Ulimwenguni zipo kazi mbalimbalia ambazo watu huzifanya bila kujali ugumu wake, kikubwa mkono uende kinywani. Ni ngumi kuelewa raha na karaha ya kazi fulani kama hauifanyi wewe, lakini zipo kazi ambazo hata kwa macho utendaji wake hufikirisha.

Ufaransa kazi ya kulinda mnara wa ‘Jumon Lighthouse’ inatajwa kuwa ndiyo kazi ngumu zaidi nchini humo kutokana na mazingira yake ya kazi kuwa katikati ya bahari. Lakini kazi hiyo inatajwa kuwa na mshahara mkubwa zaidi.

Mlinzi wa mnara wa taa au ‘Jumon Lighthouse’ hufanyakazi ya kuelekeza meli kwa ajili ya kuziepusha na ajari, ambapo mlinzi huweka mwanga sahihi ambao unawaelekeza waendesha meli.

Mshahara katika kazi hiyo ni dola 1.2 milioni kwa mwaka ambayo ni zaidi ya tsh 2.549 bilioni.

Kwa mujibu wa baadhi ya wadau wameeleza kuwa kazi hiyo ni ngumu kutokana na upweke anaokutana nao mlinzi huyo kwa sababu eneo la kazi hakuna mtu mwingine wa kuongea naye, hivyo jambo hilo linaweza kumsababishia matatizo ya afya ya akili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post