Idadi ya wakazi duniani kufikia bilioni 8

Idadi ya wakazi duniani kufikia bilioni 8

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba idadi ya wakazi duniani itafikia bilioni nane kufikia Novemba 15 na itaendelea kukua ingawa kwa kasi ndogo na kwa tofauti ya kimaeneo, katika miongo ijayo.

Makadirio hayo ni mara tatu zaidi kuliko wakazi bilioni 2.5 waliohesabiwa mnamo 1950.

Rachel Snow wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya wakazi duniani ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba licha ya kuongezeka katika miaka ya 1960, kasi ya kukua kwa idadi ya wakazi duniani imepungua kwa kiwango kikubwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags