Huyu ndio Mandonga mtu kazi amtaka Dullah Mbabe

Huyu Ndio Mandonga Mtu Kazi Amtaka Dullah Mbabe

Ebwana eeh!! licha ya kuchapwa kwa Knock Out, Karim Mandoga Amedai anatamani kucheza na bondia Abdallah Pazi maarufu ’Dullah Mbabe’pambano lake lijalo.

 Ambapo amesema ni bondia ambaye huwa anatamani kuzichapa naye kwa muda mrefu na anaamini atampa upinzani.

“Natamani kucheza na Dulla Mbabe,naamini kuna siku hili litatimia”alisema bondia huyo ambapo usiku wa kuamkia jana Jumapili alichapwa kwa KO na Shaaban Kaoneka huku akitoboa siri kipigo hicho na kuwaomba mashabiki wake kutorudi nyuma.

“Mpinzani wangu alinipiga right (ngumi ya kulia)akaunganisha left hood nikayumba, wakati natambalia mikono nikitaka kunyanyuka refarii akamaliza pambano”alisema Madonga mtu kazi

Mandonga mtu kazi alisema kuwa yuko fiti na mashabiki wake wasirudi nyuma kwani kukosea leo sio kukosea kesho.

Haya mtu wangu unaipa asilimia ngapi kali hiyo ya Mandonga mtu kazi? Dondosha comment yako hapo chini kupitia www.mwanachiscoop.co.tz


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post