Huwenda Ne-Yo yakamkuta ya Diddy

Huwenda Ne-Yo yakamkuta ya Diddy

Mama watoto wa mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Ne-Yo anayefahamika kwa jina la Big Sade amemfananisha msanii huyo na Diddy kwa kumuita 'Diddy Junior'.

Kwa mujibu wa Tmz News imeeleza kuwa mwanamke huyo amedai kuwa Ne-Yo ni mmoja kati ya watu wanaoelekea kuumbuka kama Diddy kwa tabia zake chafu .

Ne-Yo ameshambuliwa na mama huyo kwa maneno akimtuhumu kwa ukatili na kushiriki ngono mbele ya watoto wake, kujihusisha na madawa ya kulevya na unyanyasaji dhidi yake.

Hivi karibuni Sade alirekodi video ya majibizano yake na msanii huyo na kuirusha mitandaoni ambapo alitoa shutuma hizo na huwenda Ne-Yo ni mmoja kati ya wanamuziki wanaofuata kuumbuliwa nchini humo.

Msanii huyo amewahi kufanya nyimbo kama Give me Everything, Closer, Mad, So Sick, Because of You, Miss Independent, She Knows, Time of Our Lives. Pia miaka 7 iliyopita aliwahi kufanya kolabo na DiamondPlatnumz katika wimbo wa ‘Marry You’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags