Huu ni muda wa miss world kuleta taji Afrika

Huu ni muda wa miss world kuleta taji Afrika

Msimu wa 71 wa shindano la kumpata mlimbwende wa dunia (Miss World) ulianza rasmi Februari 18, 2024, na utaendelea kwa siku 21 na kufikia tamati Machi 9 nchini India.

Washiriki 120 kutoka mataifa mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na Tanzania, watashiriki katika mashindano mbalimbali na shughuli za hisani, ili kumpata mrembo mmoja atakayevalishwa taji la Miss World.

Aidha wakati mashindano hayo yanaendelea katika ukurasa wa mtandano wa kijamii wa Instagram wa Miss World waliweka kipande kifupi cha video kinachoonesha washiriki wakiwa kwenye gari wakiimba wimbo maarufu 'Waka Waka (This Time for Africa)' wa mwimbaji raia Colombia Shakira, ambao ulitoka rasmi mwaka 2010 kama wimbo rasmi wa Fainali ya Kombe la Dunia la 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Video hiyo ambayo inaonesha washiriki wimbo huo kwa furaha wenye tafsiri ya sasa ni muda wa Afrika, imeibua mijadala mbalimbali kutoka kwa mashabiki wakidai kuwa inawezekana mwaka huu taji hilo likachukuliwa na mrembo kutoka Afrika, kwani hata washiriki  wenyewe wanaonekana kutamani iwe hivyo.

Hati hivyo nchi pekee za Afrika zilizowahi kuondoka na taji hilo ni Afrika Kusini, Misri na Nigeria.

Kwa Nigeria taji hilo lilichukuliwa mwaka 2001 na Miss Agbani Darego. Afrika Kusini ilishinda taji la Miss World mwaka 1958, 1974, na 2014, huku Misri ikiibuka kidedea mwaka 1954.

Kidunia, India na Venezuela ndizo nchi ambazo zimeshinda mataji mengi zaidi ya Miss World, zote zikiwa na mataji sita hadi sasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags