Hushpuppi atapeli Milioni 926 akiwa jela

Hushpuppi atapeli Milioni 926 akiwa jela

Unaambiwa kwamba Ramon Abbas maarufu kama Hushpuppi amefunguliwa mashtaka mengine mapya ya utakatishaji fedha baada ya kufanya utapeli wa $400,000 sawa na Tsh million 926 akiwa gerezani Marekani.

Waendesha mashtaka wa Marekani waliwasilisha hati mbele ya Mahakama ya Wilaya ya California, Marekani siku ya jana Machi 16, pamoja na ushahidi kuhusiana na Hushpuppi kutenda uhalifu katika ofisi ya magereza.

Hushpuppi anadaiwa kununua kadi za benki 58 za wizi mtandaoni zenye thamani ya $400,000 ambazo hutolewaga maalum kwa ajili ya malipo kwa raia wa Marekani waliopata athari za kiuchumi kutokana na majanga kwa kusaidiana na mtu aliyejiita AJ aliyekuwa anawasiliana naye na ndiye aliyefanya malipo ya kadi hizo.

Hushpuppi alifanya harakati hizo kipindi ambacho wafungwa wanapewa nafasi ya kupiga simu, kutumia computer na mitandao ya kijamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags