Hugh Jackman agoma kueleza sababu ya kuachana na mkewe

Hugh Jackman agoma kueleza sababu ya kuachana na mkewe

Muigizaji kutoka nchini Australia, Hugh Jackman ameeleza kuwa hayuko tayari kuzungumzia sababu ya kutengana na mke wake. Hugh anaonekana kuchukizwa na maswali anayoulizwa na baadhi ya watu kuhusiana na  sababu za yeye na mkewe kuachana.

Kwa mujibu wa TMZ muigizaji huyo hakutaka kuzungumzia sababu ya kuachana na Deborra-lee ambaye alikuwa mke wake, na ndoa yao ilidumu kwa muda wa miaka 27 na ghafla ilileta taharuki kwa watu hivi karibuni baada ya kuenea taarifa kuwa  ndoa hiyo haipo tena.

Hugh wakati akiulizwa sababu za kutengana amedai kuwa hajisikii vizuri kujadili suala hilo, lakini anachotaka watu watambue ni kuwa wanapitia wakati mgumu wote wawili kukabiliana na hali hiyo ya kutengana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags