Hizi ndizo sababu za Klabu ya Simba kuikubali M-Bet

Hizi Ndizo Sababu Za Klabu Ya Simba Kuikubali M-Bet

Ceo wa Simba, Barbara Gonzalez amesema ameweka bayana sababu za klabu hiyo kuikubali M-Bet ambapo amesema kuwa moja ya jambo kubwa kabisa ni kwamba M-Bet wameweza kukidhi mahitaji  ya klabu hiyo.

“leo ni siku kubwa kwa simba na M-Bet, swali kubwa ni kwanini M-Bet, sababu kubwa ni wameweza kukidhi mahitaji yetu, washirika wote wa Simba kwa sasa wamejitoa kwa simba tu”.

“Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania”.

"Hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na senior team pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake”.

Nikukumbushe tu kuwa klabu  ya Simba sc leo imetangaza thamani ya mkataba wao wa udhamini mkuu na M- Bet kuwa una thamani ya tsh bilioni 26.1 katika kipindi cha miaka 5.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post