Hivi unajua tabia yako ipo kwenye kundi lako la damu ( part 2)

Hivi unajua tabia yako ipo kwenye kundi lako la damu ( part 2)

Aloweee!! Leo ni wikend nyingine kabisa tukimalizi malizia mwezi mtukutufu wa ramdhani I hope uko sawa ramadhani inaenda barabara kabisaa, kama kawaida wafuatiliaji wetu wa afya sasa leo bwana tunaendelea na pale tulipoishia, kuhusiana na maswala ya tabia yako kuwa kwenye damu.

Week ilioisha bwana tulizungumzia na wale wa kundi A la damu kuhusiana tabia zao, utendaji wao wa kazi, katika mahusiano, tabia mbaya na tabia nzuri walizo nazo, sasa wiki hii tunakusogezea wale wanangu wa kundi B la damu.

Damu kundi ‘B’

Kama tulivyo zungumza hapo awali tabia yako siku zote inaendana na kundi lako la damu sasa tunaangalia kwa upande wa kundi B la damu watu wa kundi hili bwana mara nyingi wanakuwa na tabia za kuasi (tabia za kigaidi) na ngumu katika jamii kuwazuia au kuwatuliza wanapofanya jambo lao.

Kundi B ni watu wanandoto na maono makubwa wanasukumwa kwa kasi na kiu zao za kufanya jambo ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu mara nyengine inakuwa ni vigumu kumzoea wana simamia sana kile wanachokiamini kwa wakati huo hata kama ulimwengu mzima upinge.

Ni watu wazungumzaji yaani ukiwapa nafasi ya kuzungumza wanaweza kuongea mpaka asubuhi na wasimalize mala nyingi unawapata katika kazi za MC au Motivation speaker. 

Mazuri na Mapungufu yao

Watu wa kundi B huwa wanasukumwa katika kufikia malengo yao wako kasi katika utendaji, wanapenda raha,wanahisia nzito,wanaya tazama maisha katika mtazamo chanya,wanaweza kujisimamia wao wenyewe bila kuongozwa na kujitegemea na hawajawahi kukubaliwa na wengine

Katika mapungufu yao watu hawa huwa ni wabinafsi na maranyinge wanakwepa majukumu yao, wagumu sana kusamehe, wasumbufu sana,wanaweza kuwa wakatili na wenye hasira za haraka.

Maisha yao katika jamii

Mara nyingine wanakuwa wagumu katika shuguli mbalimbali katika jamii hata kuwa nao nakushiriki jambo fulani maana wanapenda kufanya mambo yao wenye  wanachokiamini ni kuwa wao wenyewe wanajitosheleza hii ni kutokana na wanavyojiona katika jamii. Kiufupi watu wa kundi hili bwana tuseme tuu wanajiona ka lugha nyepesi. 

Kundi B Kazini/ ofisini

Ingawa wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kwa wasumbufu sana na wagumu katika kushirikiana nao kazini, ningumu kufanya nao kazi sehemu moja maana wapenda na kutaka kufanya kazi peke yao.

 Watu wa kundi B katika mahusiano ya mapenzi

Unaweza kufurahi nao kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla, vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia  fahamu kuwa wanaweza kukuwakia muda wowote wanao jiskia wakati mwengine bila sababu ni wakatili na wasio maanisha kile wanacho kisema huwa na ahadi za uongo.

 Baadhi ya ukweli wa kitafiti kuhusu watu wa kundi B

  • Wanatabia ya utukutu na umbea sana na kugombanisha watu wao nikitu cha kawaida
  • they love pets kupindukia mpaka kero
  • wanakinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magojwa
  • wanafurahia vyakula zaidi vitokanavyo na wanyama kama maziwa “dairy product’’

Afya yao kiujumla.

Kundi B niwatu ambao husumbuliwa au wako hatarini kupata ugonjwa kama uvimbe wa fizi na pia wanawake walioko katika kundi hii wako hatarini kupata ugonjwa wa kisukari. ( ni utafiti na sio wote wanaweza kupata ugonjwa huo)

Mara nyingi ni watu ambao wakipata virusi vya aina yoyote ile huwa wanaugua uchizi wanakuwa vichaa kabisa kutokana kwamba hivyo virusi vinaenda kuharibu mfumo wa fahamu, wanauwezekano mkubwa wa kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Watu wakundi hii hawashauri sana kula vyakula vya ina ya kuku, karanga, korosho na nyanya mara kwa mara.

Naona kama tuishie hapa ila week ijayo buan mungu akitujaalia uzima basi tutaendela na kundi AB la damu, ambalo jilo bwana ndo linamabalaa kama yote, usiache kutembelea website yetu www.mwananchiscoop.tz kama ulipitwa wiki iliopita.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags