Hii Young Famous msimu huu inaupiga mwingi sana

Hii Young Famous msimu huu inaupiga mwingi sana

Nyie nyie mjini kumechangamka haswa baada ya lile jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu Realiy show ya ‘Young, Famous, and African’ ambayo imewashirikisha matajiri na mastaa, barani Afrika sasa inaupiga mwingi hatari, ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua yanayoriojiri.

Onyesho hilo ni la Kiafrika na la kwanza la aina yake. Linalounganisha kundi la nyota mashuhuri, matajiri vijana wa vyombo vya habari kutoka katika bara zima na ushujaa wao huko Johannesburg, Afrika Kusini, wakieleza mahusiano yao, familia, maisha ya kazi, na mengi zaidi yanachunguzwa katika mchezo wa kuigiza wa maisha halisi.

Katika msimu mpya, wasanii waliorejea ni pamoja na supastaa wa Bongo Flava Diamond Platnumz; kando yake ni baby mamake wake kutoka Uganda Zari Hassan; Waafrika Kusini Khanyi Mbau; Nadia Nakai; Andile Ncube; Quinton aka ‘Uchi DJ’ Masina; Kayleigh Schwark; na Annie Macauley Idibia wa Nigeria; na Swanky Jerry.

Ili kufanya mambo kuwa ya fujo na kunogesha show hiyo, mastaa hao tisa wanajumuika na vipaji vipya vilivyo tayari kuibua mambo, akiwemo Queen B mwenyewe, Bonang Matheba, sosholaiti Sebabatso Motsibi, mwanamuziki wa Ghana na Marekani Fantana, mjasiriamali mzaliwa wa Namibia na mwenza wa zamani wa Bib Brother Africa. Luis Funana, na mwanamitindo Rosette Ncwana.

“Ninapotazama Young, Famous, na African, mimi hutulia na kuchukua dakika kadhaa kupiga mayowe hewani, kisha niendelee” anaandika shabiki mmoja kwenye Twitter.

Hisia hii haishangazi, kwani anasa, mafanikio, na majigambo mengi bado yapo kwenye menyu ya mfululizo maarufu wa TV wa Netflix.

Onyesho la uhalisia (realy show) la vipindi tisa limejazwa na mazungumzo mengi na hali ndogo katika kila sehemu ambayo haikupaswa hata kupeperushwa nje ya uwiano. Lakini hiyo ndiyo aina ya drama ambayo watazamaji wanatamani.

“Nimekuwa nikitazama Young, Famous, and African kwenye Netflix na siwezi kuamua nani ni sumu zaidi kati ya Swanky, Bonang, na Zari. Yoh, ni wengi!” Morgan anaongeza.

Mchanganyiko wa washiriki wa zamani na wapya labda umeunda kichocheo cha maafa kamili.

Kuanzia mavazi hadi magari wanayoendesha, yote ni ya kung'aa, urembo, na maigizo, lakini pia tunapata mtego juu ya maisha halisi ya watu mashuhuri wa Kiafrika, mapambano yao, wasiwasi na wahusika.

Katika kipindi cha dakika 30, baadhi ya watazamaji waliachwa wakiwa wamehuzunishwa na hadithi ya jinsi mambo ya "kidunia" yalivyomgharimu Mmibia Luis Munana uhusiano na familia yake.

“Nilipotoka katika nyumba ya Big Brother, nilitengwa na baadhi ya watu” anaongeza Luis.

Huku Golden Boy, maarufu kama Munana, alitengwa na shirika la kidini la familia yake kufuatia kipindi cha awali cha televisheni ya ukweli katika msimu wa tisa wa Big Brother Africa, ambapo alikuwa na uhusiano wa karibu na mfanyakazi wa nyumbani.

Tangu wakati huo, Munana amezuiliwa kuzungumza na familia yake, marafiki, na washiriki wengine wa shirika la kidini isipokuwa kuna mazingira ya kipekee.

Ndani ya shoo hiyo, Munana anakiri kuwa anawakosea, na kuna mengi anatamani kuwashirikisha.

Yaani unaambiwa 15 ya watu mashuhuri wa orodha ya A Afrika wana urembo, utajiri, akili, lakini adabu ya kimsingi haiko kwenye taswira zao. Wanawake, wanaojiita 'Malkia', wanapigana juu ya mwanamume ambaye hapendezwi sana na yeyote kati yao.

“Young, Famous, and African is just back-to-back drama! I'm like, Lawd, y'all can't have one adecent conversation,” alitoa maoni Diana Nae.

Msimu wa pili ni mzuri; baadhi ya mienendo hubadilika, na mpangilio mrefu wa msimu unatoa nafasi kwa kila mtu kukua kwa kila hali anayokabiliana nayo.

Mchezo wa kuigiza unaweza kuwa mwingi, lakini inachekesha sana kuona wanachosema kila mmoja na jinsi wanavyotendeana wanapokuwa na suala. Kila mshiriki ana utu dhabiti, na watazamaji wanaweza kujifunza kutoka kwao.

Athari nyingine inayoonekana ni kwa Chibu Dangote. Kuimarika kwa Diamond Platinum katika Kiingereza kumewafanya mashabiki na wafuasi wake wengi kushangaa katika msimu wa pili.

"Niko hapa kwa ajili ya kuboresha Kiingereza cha Diamond," shabiki mmoja kwa jina Maggie alitoa maoni.

Akijulikana kwa nyimbo zake maarufu, zikiwemo ‘Iyo’, ‘Waah,” na nyinginezo nyingi, msimu wa kwanza wa Diamond, hata hivyo, ulikabiliwa na ukosoaji wa Kiingereza chake huku akihangaika kutoa sentensi.

Lakini Simba ilikuja kuwa mkubwa na bora zaidi msimu huu wa pili. Kuonyesha mashabiki kwamba alihudhuria masomo yake na kupata kitu.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags