Haya ndiyo yatakufanya utoboe kimaisha 2024

Haya ndiyo yatakufanya utoboe kimaisha 2024

 Najua wiki hii siyo ya kuongelea kazi lakini sina budi kuwajuza jambo hili dogo kabisa ambalo halitawachosha kabisa,  leo katika kazi tutazungumzia suala la malengo yako kwa mwaka ujayo, umejipangaje, umeshaandika malengo yako unayotaka kuyafanya 2024.

Malengo ni mipango ambayo inawekwa kwa ajili ya kutimizwa/kufikiwa  katika muda fulani,  ili malengo yako yaweze kutimia unatakiwa kuyaheshimu kwani usipofanya hivyo hayawezi kutimia.

Kwa watu mbalimbali hasa wenzetu wa mataifa mengine ifikapo mwisho wa mwaka hununua diary na kuanza kuandika yale yote ambayo mtu anatamani kuyafanya kwa mwaka unaofuata ili aweze kuimarisha maisha yake, nawe pia rafiki yangu unayesoma makala hii unahitaji kufanya hivyo kwa sababu bado haujachelewa na hii itakusaidia kufanya kazi kwa bidii ili kuyatimiza

Kitu muhimu ninachopenda kukumbusha hapa ni kwamba ukiweka malengo basi jitahidi kuyaheshimu kwani usipoyaheshimu hutayatimiza na utayaweka kando kwani utakuwa na visingizio au sababu lukuki za kutofikia malengo.

Hichi ndicho kitafanya utimize malengo yako kwa mwaka 2024.

  • Kumtanguliza Mungu kwa kila jambo
  • Kuamini na kuweka akilini kuwa yote yanawezekana, hakuna aliyezaliwa anajua na wala hakuna aliyezaliwa amefanikiniwa hata hao waliofanikiwa walijiwekea malengo kama unavyofanya wewe.
  • Kutotoka ndani ya malengo yako, hii niielezee kidogo kuna baadhi ni wepesi sana wa kuandika malengo lakini kuyatimiza yanakuwa mtihani, mwaka ukichanganya anasahau yote aliyojiwekea na kuanza kufanya vitu visivyo eleweka, jitahidi kutimiza ahadi zako mwenyewe.
  • Kutojiwekea malengo makubwa usiyoweza kuyatimiza na ndiyo maana utajiri unatofautiana hivyo basi katika kujipangia malengo yaandike yale yaliyo ndani ya uwezo wako na yanayo endana na kipato chako.
  • Malengo yasiwe mateso kwako jipe muda wa kufurahi, kutimiza malengo ni kama kufanya mtihani tu kuna muda utasoma na kuna wakati utafurahi na marafiki, kufurahi na ku-enjoy itakusaidia kupata knowledge mpya itakayo kusaidia kufikia malengo yako.

Hata kama huna ajira usiache kujiwekea malengo kwa sababu siku zote ‘Mungu huumpa mja amtaka’ inawezekana mwaka ukaanza tu na kupata kazi, sawa sasa hivi hauna kipato lakini usiache kujiwekea malengo cha kuzingatia zaidi kutokuchagua kazi, mfano umesomea sheria basi lazima uwe mwanasheria sometime tunasoma kama daraja tu la kufika sehemu fulani.

Wapo ambao watadharau suala hili lakini ndiyo jambo kubwa ambalo litakufanya utoboe kimaisha mwaka 2024, kwa sababu siku zote waswahili wanasema ‘Mali bila daftari huisha bila habari’ ukijiwekea malengo yatakusaidia na utakuja kunishukura baadaye hata kama ni lengo moja wewe weka tu na ujue kabisa lazima ulitimize.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags