Hatimaye Drake aifikia record ya Michael Jackson

Hatimaye Drake aifikia record ya Michael Jackson

Hatimaye Rapa kutoka nchini Marekani Drake ameifikia rekodi ya Michael Jackson kwenye charts kubwa za muziki duniani #BillboardHot100, ni baada mwanamuziki huyo kufikisha ngoma 13 ambazo zimeshika namba moja kwenye charts hizo.

Ambapo hapo awali ilikuwa inashikiliwa na marehemu Michael Jackson, na sasa Drake ameifikia baada Ya wimbo yake ‘First person shooter’ aliomshirikisha #Jcole kushika namba moja kwenye charts hizo wiki hii .

Drake kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza furaha yake baada ya kufikia rekodi hiyo na amedai kuwa alitakiwa awe ameivunja rekodi hiyo kitambo lakini kwa kuwa hakupewa credit kwenye ngoma ya Travis Scott "Sicko mode" basi amechelewesha kuivunja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags