Hatimaye Cardi B ajifunza kuendesha gari

Hatimaye Cardi B ajifunza kuendesha gari

Baada ya kumiliki magari ya thamani kwa muda mrefu ambayo hajui kuyaendesha, hatimaye mwanamuziki kutoka nchini Marekani Cardi B, ameanza kujifunza namna ya kuendesha gari akiwa na miaka 31.

Kwa mara ya kwanza akiwa kwenye mafunzo ya uendeshaji gari, aliingia kwenye Instalive akionesha mashabiki wake akiwa na mwalimu ambaye anamfundisha namna ya uendeshaji, kwa kutumia gari yake aina ya Rolls-Royce.

Hata hivyo Cardi ameeleza kuwa daktari wake amemshauri kujifunza vitu vipya kwa ajili ya kuweka afya yake sawa, hivyo ameeleza kuwa kila siku atatumia saa moja kwa ajili ya kuendesha gari.

Baadhi ya magari anayomiliki Cardi ni Lamborghini Aventadors, Bentley Bentayga, Lamborghini Urus, Rolls-Royce Wraith, Dodge Challenger Hellcat, McLaren 720S Spider, Lamborghini Huracan na Ferrari Portofino.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags