Harmonize atupa dongo gizani, Amtania Ibraah

Harmonize atupa dongo gizani, Amtania Ibraah

Mwanamuziki wa #BongoFleva, Harmonize amefanya utani kwa #Ibraah ambaye ni msanii anayemsimamia katika lebo yake ya Konde Gang akimwambia kuwa yeye ndiyo amemtoa kimuziki.

Harmonize ameyasema hayo masaa 15 yaliyopita kupitia video aliyoi-post kwenye #Instastory yake ikimuonesha yupo na Ibraa akimfanyia utani huo akionyesha kuwa na yeye anacho cha kujivunia katika kazi yake ya muziki.

Ikumbukwe hivi karibuni msanii Diamond Platnumz alitumia kauli hiyo wakati wa tamasha la Bite Vibe akisema mbele ya mashabiki kuwa anajivunia kuwatoa baadhi ya wasanii katika lebo yake akiwemo Harmonize ambaye kwa sasa anamiliki lebo yake ya Konde Gang jambo lililozua mvutano katika mitandao ya kijamii.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags