Harmonize adai kuwa alipigwa, amtaja Kajala

Harmonize adai kuwa alipigwa, amtaja Kajala

Si kawaida ya Harmonize kumsema mtu kwa kumtaja jina zaidi hutumia mafumbo na wakati mwingine huwasilisha ujumbe kwa njia ya nyimbo, sasa baada ya uvumiliu kumshinda #KondeBoy ameamua kutoa ya moyoni huku akilitaja jina na Kajala.

Baada ya ukimya wake leo kaamua kufichua yale yaliyokuwa yamejificha kwa kudai kuwa Kajala alikuwa haamini kama licha ya ugomvi wote bado mmakonde muachia gari.

Katika walaka wake Harmonize ambao ameuandika kwenye #InstaStory yake amedai kuwa dear ex #Kajala anapokuwa akisema kuhusu mabaya yake basi aseme na mazuri ambayo amewahi kumfanyia, huku Harmonize akidai kuwa amewahi kumsaidia mzee Masanja ili asifungwe.

Harmonize amedai kuwa alirushiwa matusi na kupigwa,kama alivyoelezea kweye wimbo wake mpya uitwao Ex kuwa akilewa ataongea zaidi, na kwenye walaka alioandika #Insta amerudia tena kauli hiyo ya akilewa atazungumza zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags