RHOBI CHACHA
Ni nani atakayeibuka mshindi wa tuzo za Hollywood and African Prestigious Awards (HAPAWARDS)?
Ni swali linalosubiriwa kujibiwa kwenye usiku wa kinyang'anyiro cha tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika nchini, kwenye Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, Agosti 10, mwaka huu na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Kedmon Mapana amesema tuzo hizo zimegawanyika katika vipengele vikuu vitatu vya Muziki, Mitindo na Filamu na kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu, wametangaza rasmi majina ya wasanii na wadau wa sanaa wanaowania tuzo hizo na zinafanyika kwa mara ya kwanza nchini.
Amesema kutakuwa na vipengele 11 vya muziki, 21 vya mitindo na 11 kwa upande wa filamu, huku cha muziki watashindanishwa wasanii wa muziki wa Dansi, Singeli, Taarabu pamoja na Ngoma za Asili.
“Lengo la tuzo hizo ni kuendelea kuwajenga Wasanii na kuwapa fursa ya Kujulikana kimataifa, hivyo kutakuwa na vipengele vya Muziki, Mitindo na Filamu.
“Majaji watakuwepo kutoka Marekani na wengine kutoka hapa Tanzania watakaofanya mchujo katika vipengele hivyo hadi kutapa mshindi, kutakuwa na Vipengele vya Muziki 11, 21 Fashioni pamoja na vipengele Filamu 11,” amesema Mapana.
Tuzo hizo zimekuwa zikitolewa kwa miaka saba mfululizo Marekani na kwa mwaka huu zinafanyika kwa mara ya kwanza Afrika zikihusisha pia wasanii wa Marekani katika vipengele mbalimbali kama filamu bora, mwigizaji bora wa kike na kiume, wasanii bora wasaidizi, wachekeshaji bora, tamthilia bora na vingine vingi.
Mwenyekiti wa tuzo hizo kwa upande wa hapa Tanzania Mrisho Mrisho alivitaja vipengele hivyo na wasanii wake ni;
KIPENGELE CHA MUZIKI
1: Msanii Bora Chipukizi (Bongo Fleva, Tanzania)
-Yammi
-Vannillah
-Founder Tz
-Mrs Energy
-Aslam TZ
2. Msanii Bora (Muziki wa dansi, Tanzania)
-Malaika Band
-Twanga Pepeta
-Msondo Ngoma
-Mlimani Park Orchestra
-Mjengoni Band
3. Msanii Bora (SINGELI, TANZANIA)
-Dulla Makabila
-D Voice
-Sholo Mwamba
-Meja Kunta
-Wamoto Band
4. Msanii Bora (TAARAB, TANZANIA)
-Nakshi Nakshi Band
-Jahazi Modern Taarab
-Blue Stars Modern Taarab Band
-Tam Tam Band
-First Class Modern Taarab
5. Msanii Bora Muziki wa Injili, TANZANIA)
-Zabron Singers
-Neema Gospel Choir
-Agape Gospel band
-Joel Lwaga
-Rose Mhando
6. Msanii Bora (Muziki wa kitamaduni, Tanzania)
-Mrisho Mpoto
-Saida Karoli
-Awilo Kidume cha Mbeya
-Wamwiduka Band
-Nyati Group
7. Msanii Bora (HIPHOP, TANZANIA)
-Darassa
-Young Lunya
-Rosa lee
-Stamina
8. Msanii Bora wa kike wa kimataifa anayechipukia
-Abigail Chams (Tanzania)
- Nina Roz (Uganda)
- Nikita Kering (Kenya)
-Winnie Nwagi (Uganda)
-Belle Aire (United States)
9. Msanii Bora wa Kiume Afrika
-Tay Grin (Malawi)
- Romeo Mputu (Congo)
-RJ Kanierra (Congo)
-Bien (Kenya)
10. Kundi Bora la Kimataifa
-Jasper Boyz (South Africa)
-Sarah Lula (Congo)
-Fred Kabeya (Congo)
11. Msanii Bora la Kimataifa la Hip Hop
-NAVIO (Uganda)
-Pharaoh (USA)
-MC Baba (Congo Brazzaville)
-Nezaboy (Nigeria)
B. KIPENGELE CHA MITINDO
12. Mbunifu Bora wa Mavazi wa Kike (Tanzania)
-Kiki Zimba
-J’adore Couture
-Khadija Mwanamboka
-Hasia Hidalus
13. Mbunifu Bora wa Mavazi wa Kiume (Tanzania)
-Kulwa Mkwandule’son
-Chuwa fashion
-Zado fashion
-Mustafa Hasanali
-Ally Remtula
14. Mbunifu Bora wa mavazi/Mwanzilishi (Tanzania)
-Ekantik
-Kingasira Zanzibar
-Sheria Ngowi
-Johary Jafary Kisoma
15. Mwanamitindo Bora wa kike (Tanzania)
-Glory Monyo
-Anitha Mlay
-Herieth Paul
-Flaviana Matata
-Miriam Odemba
16. Mwanamitindo Bora wa Kiume (Tanzania)
-Kenny Kaiser
-Ibrahim Maumba
-Thomas Nguka
-Simo Poluse
-Ally Chamas
KIPENGELE CHA FILAMU
17. Filamu Bora Ndefu 'Tamthilia' (AFRICA)
-JUA KALI (LEAH MWENDAMSEKE)
-HUBA (AZIZ MOHAMED)
-KOMBOLELA (ABDUL USANGA)
-BUNJI (ISARITO MWAKALINDILE)
-EZRA (LEAH MWENDAMSEKE)
18. Filamu Bora Ndefu (AFRICA)
-Jua Kali (Leah Mwendamseke)
-Huba (Aziz Mohamed)
-Kombolela (Abdul Usanga)
-Bunji (Isarito Mwakalindile)
-Ezra (Leah Mwendamseke)
19. Filamu Bora Ndefu (Africa)
-Jungwa (Benard Edson)
-Mateka (Sayusi)
-Binti (Seko Shamte)
20. Mwangozaji Bora wa Filamu (Africa)
-Leah Mwendamseke (Jua Kali)
-William Mtitu (Slay Queen)
-Vicent Kigosi (Jeraha)
21. Mwigizaji Bora wa Tamthilia za TV (Africa)
-Salim Ahmed (Gabo) (Baba Olivia)
-Single Mtambalike (Jeraha)
-Hussein Lugendo (Nuru)
22. Mburudishaji Bora wa TV (Africa)
-Wensekula Lotti
-Nasma Hassan Athumani (Nana Dolly)
-Sayeed Zuberi (Kimbembe)
23. Mwigizaji Bora wa Kike wa Tv (Tanzania)
-Blandina Chagula
-Welu Sengo
-Mariam Ismail
24. Mwigizaji Bora wa Kike wa TV- Tamthilia (Africa)
-Yobnesh Hassan (Mawio)
-Jeniffer Kyaka (Fungu Langu)
-Miriam Robert (Toboa Tobo)
25. Mwigizaji Bora Msaidizi wa Kiume wa Tv - Tamthilia (Africa)
-Abbort Charles (Juakali)
-Fredy Kiluswa (Slay Queen)
-Hussein Nawanda (Zahanati Ya Kijiji)
26. Mwigizaji Bora Msaidizi wa Kike wa Tv - Tamthilia (Africa)
-Elizabeth Michael (Jua Kali)
-Halima Yahaya (Single Mama)
-Irene Paul (Siri)
27. Mwigizaji Bora wa Kike wa Filamu Ndefu (Africa)
-Godlive Godian (Binti)
-Irene Uwoya (Olema)
-Christina Mroni (Fumbuo)
28. Mwigizaji Bora wa Kike wa Filamu Ndefu (Africa)
-Idris Sultan (Married To Work)
-Salmin Ismail Hoza (Kusa) (Kande Khampala)
-Steven Almas (The Green Tanzanite)
29. Mwigizaji Bora Msaidizi wa Kike wa Filamu Ndefu (Africa)
-Neema Walele (Sweta)
-Sauda Simba Kirumanga (Binti)
-Regina Mroni (Fumbuo)
30. Mwigizaji Bora Msaidizi wa Kiume wa Filamu Ndefu (Africa)
-Collins Frank (It Still Okay To Date)
-Daudi Michael (Kesho Yangu)
-Shikunzi Haonga (Kitovu Cha Kifo)
31. Mpigapicha za Video Bora (Africa)
-Fredy Feruz (Dosari)
-Adam Juma (The Green Tanzanite)
-Stanford Kihore (Online)
32. Mchekeshaji Bora (Africa)
-Lucas Mhuvile (Joti) (Maharage Ya Mbeya)
-Emanuel Masanja Original Comedy Program)
-Martine White (Nazi Bubu)
33. Mwigizaji Bora wa Kike wa Kimataifa
-Cassie Kabwita (Zambia)
-Jaqueline Fleming (Usa)
-Matilda Lambert (Nigeria)
-Monica Swaida (Nigeria)
34. Washereheshaji Bora (Tanzania)
-Gala B
-Dr. Chris Mauki
-Mc Big
-Dr. Cheni
-Anjela Bondo
35. Tuzo ya Mafanikio ya muda wote kwenye Burudani
- Gabriel Mtitu (Mtitu Games)
36. Msanii Bora wa Mapambo 'Upambaji'
-Kamille Marie Artis
37. Mwanamke Bora wa Mwaka wa Kimataifa
-Rais, Dr. Samia Suluhu Hassan
Leave a Reply