Hanscana ammwagia sifa Diamond

Hanscana ammwagia sifa Diamond

Mtayarishaji wa video za muziki nchini Hanscana ammmwagia sifa msanii Diamon kwa kuipigani tasnia ya muziki wa Bongo.

Wakati akimtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa Hanscana ameweka wazi kuwa Diamond aliwahi kumsafirisha kwenda katika nchi mbalimbali ili kujifunza kurekodi video zenye ubora.

“Kikafanyika kikao kirefu sana ni namna gani tunaweza tengeneza music video kali ndani ya nchi yetu zenye hadhi ya kimataifa? na sio kutegemea video toka mataifa mengine moja ya vitu nilivyomuomba ni anipe nafasi ya kushiriki katika video zake zinazoshutiwa na ma-directors wa nje ya tanzania then nikiona wanachofanya ndiyo nitakuja na solution.

“Basi akawa ananisafirisha kwa hela zake ili nikajifunze aka ni-link na Godfather wa S.A na directors wengine wakubwa Africa, yote hiyo ni kwa manufaa ya industry nzima, baada ya kujifunza kama mwaka mzima nikarudi kufundisha directors wengine the rest is history now tunazalisha videos kali kulipo nchi yoyote Afrika Mashariki na kati na hamna tena ushamba wa ku-shoot SA,” ameandika Hanscana kwenye ukurasa wake wa Instagram

Hanscana amekuwa akifanya kazi na Simba kwa muda mrefu akiwa amemtayarishia video za ngoma kama Iyo, Oka, Naanzaje na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags