Hakuna S bila O, Vesi hii kila mtu alikariri

Hakuna S bila O, Vesi hii kila mtu alikariri

Mtazamo. Wimbo wa Afande Sele, na wale 'Bigi Mani' wenzake kwenye 'gemu'. Solo Thang Ulamaa na Prof. Jay The Heavy Weight Mc. Kilinuka sana humo ndani chini Producer Majani. Noma!

Solo ndiye aliyefungua njia. Na vesi yake tamu, ambayo kila mstari ni 'pachilaini'. Wote walitisha 'bati' humo ndani Ulamaa aliua zaidi. Hakutaka kupita ndeeefu ili kufikisha ujumbe wake.

Kwa nyakati zile kila mchizi muziki kweli, alikariri mstari kwa mstari ya 'vesi' yake. Ungependa kusikia akichana bila 'biti'. Na pia ungevutiwa na 'biti' ya Majani vile inavyomuita. Naye kuipokea kwa sauti zito.

Solo aliua kwa 'meseji' nzuri ilionyooka. Staili ya kuchana 'vesi' yake na zaidi ni ile sauti yake yenye mamlaka. Pini kubwa na 'vesi' ya Solo ni kubwa zaidi. Ilivutia kumtazama jukwaani.

Kutoka vidato sita alivyopitia. Hadi Binti akalale na Producer. Na kila Prizenta wa redio kuwa meneja wa msanii. Na dhana ya 'rapu' ni uhuni kuletwa na wa katuni. Ilibaki kubwa ni mtazamo wake tu wa fani.

Hii ni 'ova dozi' na moja ya nyimbo bora zaidi ya 'hipapu' kwa Bongo. Yes! sasa ukiunganisha na ile 'vesi' ya Prof. Jay na mwenye wimbo Afande Sele, inabaki kuwa 'ze besti hipapu songi eva'.

Solo Thang anabaki kuwa 'Kipaji kikubwa ndani ya chumba cha kuzalisha masikini. Uwezo wa Solo ni wa juu sana. Tatizo ni kukosa akili ya juu ambayo ingegeuza kile kipaji kuwa utajiri. Solo akasepa Ulaya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post